34-Adabu Za Ndoa Katika Sunnah Iliyotakasika: Haitakiwi Kulipa Swawm Ya Sunnah

 

 

Mtu akiamua kufungulia Swawm ya Sunnah, sio lazima kwake kuilipa siku hiyo. Kuna Hadiyth mbili kuhusu mas-ala haya:


Kwanza:

عن أبي سعيد الخُدْرِيِّ أنه قالَ: صَنَعْتُ لرسولِ الله صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ طعاماً فَأَتَانِي هو وَأَصْحَابُهُ، فَلمَّا وُضِعَ الطعامُ قالَ رجلٌ من القومِ: إنَّي صائمٌ، فقالَ رسولُ الله صَلَّى الله عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((دَعَاكُمْ أَخُوكُمْ وَتَكَلَّفَ لكُمْ))، ثم قالَ لَهُ:  ((أَفْطِرْ وصُمْ مكَانَهُ يوماً إنْ شِئْتَ))

Kutoka kwa Abu Sa'iydil-Khudriy ambaye amesema, "Nilimtayarishia chakula Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ambaye alikuja pamoja na Swahaba zake. Kilipowekwa chakula mmoja wao akasema: 'Nimefunga'. Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akasema: ((Ndugu yako amekualika na ametayarisha chakula kwa ajili yako)). Kisha akasema ((Fungua Swawm yako kisha funga siku nyingine badala yake ukipenda))[1]


Pili:

عن أبي جحيفة أن رسول الله صلى الله عليه وسلم آخى رَسُولُ الله بَيْنَ سَلْمَانَ وَأَبي الدَّرْدَاءِ فَزَارَ سَلْمَانُ أَبَا الدَّرْدَاءِ فَرَأَى أُمَّ الدَّرْدَاءِ مُتَبَذِّلَةً. فقَالَ: مَا شَأْنُكِ مُتَبَذِّلَةً قَالَتْ: إِنَّ أَخَاكَ أَبَا الدَّرْدَاءِ يقوم الليل ويصوم النهار  لَيْسَ لَهُ حَاجَةٌ فِي الدُّنْيَا، قالت: فَلَمَّا جَاءَ أَبُو الدَّرْدَاءِ فرحب به، وقَرَّبَ إليه طَعَاماً فَقَالَ لَهُ سُلَيْمَان: كُلْ: قال: َإِنِّي صَائِمٌ. قالَ: أقسمت عليك لتفطرنه مَا أَنَا بآكلٍ حَتَّى تَأْكُلَ، قالَ فَأَكَلَ معه ثُمَّ بات عِنْدَهُ. فَلَمَّا كَانَ من الَّليْلُ  أراد أبو الدرداء أن يقوم، فمنعه سلمان وقال له: إِنَّ لِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقّاً، ، وَلِرَبكَ عَلَيْكَ حَقّاً ، [ولضيفك عليك حقا]، وَلأَهْلِكَ عَلَيْكَ حَقّا  صُمْ، وَأفْطُرْ، وَصَلّ، وَائتِ أَهْلَك، وَأعْطِ كُلِّ ذِي حَق حَقَّهُ، فَلَمَّا كَانَ فِي وَجه الصُّبْح، قال: قُمْ الآَنْ إِنْ شِئْتَ، قال: فَقَاما فَتَوَضَّآ، ثُمَّ رَكَعا، ثُمَّ خَرَجا إِلَى الصَّلاةِ، فَدنا أبُو الدَّرْداَء لِيُخْبِرَ رسول الله صلى الله عليه وسلم بِالَّذي أَمَرَهُ سَلْمَان، فَقال لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم  (( يَا أَبا الدَّرْداء! ِإنَّ لِجَسَدِكَ عَلَيْكَ حَقاً )) مِثْل مَا قاَل سَلْماَن ( وفي رواية): ((صَدَقَ سَلْمَانُ)) 
  

Imetoka kwa Abu Juhayfah رضي الله عنه, kwamba Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwaunga Salmaan رضي الله عنه na Abu Ad-Dardaa رضي الله عنه katika udugu wa Kiislam. Abu Juhayfah alisema: "Salmaan alikuja kumtembelea Abu Ad-Dardaa, na akamuona Ummu Ad-Dardaa (mke wa rafiki yake) yuko katika hali isiyo nzuri na alikuwa amevaa nguo zilizo chakaa Akamuuliza: Vipi mbona uko katika hali hiyo Ummu Ad-Dardaa? Akasema: 'Ndugu yako Abu Ad-Dardaa anakesha usiku katika Swalah na mchana anafunga na hahitaji chochote katika mambo ya dunia". Kisha Abu Ad-Dardaa akaja, akamkaribisha ndugu yake na akampa chakula. Salmaan akamuambia: 'Kula'. Lakini Abu Ad-Dardaa akasema: 'Nimefunga'. Salmaan Akasema: 'Naapa ya kwamba ni lazima ufungue Swawm yako. Sitokula hadi ule'. Kwa hiyo akala pamoja naye. Salmaan akalala usiku nyumbani kwake, na Abu Ad-Dardaa alipoamka usiku kuswali, Salmaan akamzuia na akamuambia: 'Ewe Abu Ad-Dardaa, mwili wako una haki juu yako, Mola wako Ana haki juu yako, wageni wako wana haki juu yako, na mke wako ana haki juu yako. Funga lakini pia fungua, swali (usiku) lakini pia muendee mke wako, na kila mmoja mpe haki yake'. Ilipofika karibu na Alfajiri, Salmaan akamuambia: 'Inuka sasa ukipenda'. Kisha wote wawili wakafanya wudhuu, wakaswali, na wakaenda kuswali msikitini. Abu Ad-Dardaa alipomkaribia Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kumuambia kuhusu amri ya Salmaan kwake, Mtume صلى الله عليه وآله وسلم akamwambia, ((Ewe Abu Ad-Dardaa, hakika mwili wako una haki juu yako)) Kama alivyosema Salmaan. Katika riwaaya nyingine alisema, ((Salmaan amesema ukweli))[2]



[1] Al-Bayhaaqiy na At-Twabaraaniy: Hasan

[2] Al-Bukhaariy, At-Tirmidhiy na Al-Bayhaaqiy

Share