06-Uswuul Al-Fiqhi: Asili Na Maendeleo Ya Uswuul Al-Fiqh
Sio rahisi kulisoma somo la Uswuul al-Fiqh na maendeleo yake bila ya kupitia kumbukumbu za Fiqhi. Mafundisho ya vitendo kwa Shariah ambazo yamekusanywa kusanywa kutokana na vyanzo mahsusi vya sheria.
Kubuni maana ya Uswuul ni: shina, au asili Aswl, wingi Uswuul au kile chengine ambacho kinajengwa juu yake. Kwa mfumo wa kisheria za Kiislamu (ndipo) Fiqhi inapojengwa hapo, na mizizi kutoka kwenye mashina ya Uswuul ambayo yanakuwa na chanzo chake cha ushahidi. Matokeo yake, ili kufahamu asili ya Uswuul al-Fiqh, tunahitaji kuwa na uoni wa jumla juu ya historia ya Sheria za Kiislamu. Tashri’iy
Kuanzisha vifungu vya Shariah, kuamuru sheria kufuatwa, kuweka kanuni na amri, na kufafanua miundo ni kazi ambayo ni maalumu kwa Allaah pekee. Yeyote anayejipa na kuandikia kazi hizi zaidi ya Allaah, ametenda dhambi ya Shirk. Kwani, kufanya hivyo amekwenda kinyume kabisa na imani ya Upweke wa Allaah. Tawhiyd.
Allaah Ameweka na kugawa thibati na vyanzo vilizo wazi za ushahidi kwa ajili ya kwamba; waumini wasiwe na matatizo kutafuta muongozo wao kwenda kwenye vipengele vya Sheria Zake. Au Ahkaam kwa kutumia baadhi ya vyanzo hivi vya ushahidi. Ummah wa Kiislamu umekubaliana juu ya usahihi na uhusiano wake kwa Ahkaam, na wameukubali hivyo hivyo. Hata hivyo, kuna tofauti nyingi kwa mnasaba wa vyanzo vyengine vya ushahidi.
Vyanzo vya ushahidi ambavyo Ummah wote wamekubali, na juu ya usahihi wa ambao kuna makubaliano ya jumla, inajumuisha vyanzo viwili, ambavyo vinafanya msingi wa sheria kipindi cha Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Vyanzo hivi viwili vya sheria ni:
1) Qur-aan: Hii inaweza kutafsiriwa
2) Sunnah: Inajumuisha kila kitu, nje ya Qur-aan. Ambayo imefikishwa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alilolisema, kutenda au kukubaliana nalo.
Hivyo, kila tamko la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), zaidi ya Qur-aan, na kila kitendo chake. Kuanzia mwanzo wa kazi yake mpaka mwisho wa siku zake, zinahusisha Sunnah yake. Kwa maneno ya jumla kila neno aidha linaanzisha uamuzi ambao unatumika kwa wafuasi wa Ummah wote, au uamuzi ambao unamhusisha Mtume mwenyewe peke yake au kwa Swahaaba zake wengine.
Bila ya kuangalia
Kipindi cha maisha ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maamuzi yote ya kisheria Ahkaam za Shariah, ukiunganisha na migawanyo yote,
3) Ijtihaad: Ilikuwa ikifanyiwa kazi na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na wale Maswahaba zake ikiwa na mwelekeo wa kisheria ujulikanao
Ijtihaad iliyofanywa na Maswahaba, daima ilikuwa ni kujibu mazingira ambayo yametokea kwao. Baadaye, walipokutana na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), wataeleza kilichotokezea na kumwambia walichotolea uamuzi. Mara nyengine, yeye (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anazikubali Ijtihaad zao, na uamuzi
Hivyo, tunaweza kusema kwamba; kwa hatua hiyo sheria ilitegemea kwenye mifumo miwili ya Uteremsho Mtukufu. Wahyi:
- Uteremsho uliosomwa, Wahy Matlu, au Qur-aan yenye ukamilifu isiyoigika I’jaaz.
- Uteremsho usiosomwa. Wahy Ghayr Matlu, au Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Hakika, Ijtihaad iliyofanywa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) itakuwa ni yenye kufuatwa (precedent) kwa Swahaaba zake na baadaye Waislamu. Ambazo kwa uwazi inathibitisha uhalali wa Ijtihaad, ili kwamba pale watakaposhindwa kupata uamuzi ulioamuliwa kwa kisheria ndani ya Qur-aan au Sunnah, walihitajika kufanya kazi ya Ijtihaad ili kufikia kwenye hukumu peke
Juu ya hivyo, labda ili kuipa nguvu na kuianzisha dhana hii, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwaamrisha baadhi ya Maswahaba zake kufanya Ijtihaad kuhusiana na mambo fulani akiwepo yeye mwenyewe. Kisha atawaambia nani alikuwa sahihi na nani alikosea.