07-Uswuul Al-Fiqhi: Taratibu Za Kupata Hoja Kutoka Kwenye Vyanzo
Ama kwa Quraan…
Qur-aan ilisomwa na kueleweka kwa Swahaaba bila ya wao kuhitaji msaada wa kuhitaji kukimbilia katika kanuni rasmi za sarufi. Vile vile, wamejaaliwa kuwa na muoni ulio msafi, akili za uwerevu na zilizo makini. Walikuwa na uwepesi wa kufahamu malengo ya Mtoa Sheria (Allaah) na hekima zilizomo ndani ya Sheria Zake.
Hakika ni mara chache Maswahaba walikuwa wakimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusiana na jambo lolote isipokuwa yeye mwenyewe alitaje kwanza.
Imesimuliwa kwamba Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alisema “Sijapata kuona watu bora kuliko Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Kupitia kipindi cha kazi yake, mpaka alipofariki. Wamemuuliza kuhusiana na mambo kumi na tatu, yote ambayo yametajwa ndani ya Qur-aan. Kwa mfano [maana ya]:
“Wanakuuliza (hukumu ya) kupigana vita katika miezi mitakatifu…” [2:217)
na “Wanakuuliza juu ya hedhi….” (2:222)”
Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhuma) alisema, “Walikuwa wakimuuliza yeye kwa mambo ambayo yalikuwa na azma ya uhakika kwao[1].”
Ibn ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma) kwa hili alisema: “Usiulize kwa jambo ambalo halikutokezea, kwani mimi nimemsikia baba yangu ‘Umar Ibn al-Khattwaab akisema: Mlaani yule aliyeuliza jambo ambalo halikutokezea.[2]”
Qaasim (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema (kukiambia kizazi cha tatu cha Waislamu): “Munauliza kuhusu vitu tusivyowahi kuuliza, na kugombana kuhusu vitu ambavyo hatujawahi kugombana navyo. Hata munauliza kuhusu vitu ambavyo mimi sina maarifa navyo. Lakini kama tutajua, haitoruhusiwa kwetu kubakia kimya kuhusiana navyo[3].”
Ibn Is-haaq (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Nimekutana na zaidi ya Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuliko mtu mwengine yeyote, na sijapata kuwaona watu walioishi maisha ya kawaida au ambao ni wachache wa kudai juu
‘Ubaadah bin Nusay al-Kindi (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema: “Nimejuana na watu ambao ugumu wao haukuwa imara
Abu ‘Ubaydah (Radhiya Allaahu ‘anhu) alisema ndani ya kitabu chake cha Majaaz al Qur-aan: “Haikuwahi kusimuliwa kwamba Swahaabah yeyote alikwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa elimu yoyote ambayo inawezekana kupatikana ndani ya Qur-aan[6].”
Ama kuhusu Sunnah…
Sehemu ya Sunnah ambazo zina lafudhi za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) zilikuwa ndani ya lugha za Maswahaba, hivyo walitambua maana zake na kuelewa maneno yaliyomo ndani ya aya (phrase) na yale maneno mengineo ambayo hudhihirisha maana yake (context).
Namna ulivyo mwenendo wa Mtume, waliweza kushuhudia (huo mwenendo), baadaye kuwaambia wengine vile vile
Watu walisikika wakimuuliza Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutoa Fataawa kuhusiana na masuala tofauti, na alifanya hivyo. Kesi zilipelekwa kwake, na yeye alitamka hukumu. Matatizo yatatokea miongoni mwa Maswahaba, na yeye alitoa jibu la hakika. Aidha matatizo hayo yalihusiana na mahusiano ya pamoja, tabia binafsi, au masuala tofauti ya kisiasa. Walishuhudia mazingira yote haya na walifahamu maana (ya mazingira yaliyotokea).
Watu walimuona namna Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa akiona tabia za Maswahaba wake na wengineo. Hivyo,
Juu ya hivyo, simulizi zote kuhusiana na Fataawa za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), maamuzi na kukubali au kutokubali baadhi ya masuala inaonesha kwamba yalitokea mbele ya watu wengi. Ni kama mfano wa anavyotambua daktari na wenziwe, kutokana na mjumuiko wa muda mrefu na kutambua wenyewe mazoea[7] sababu za yeye kuelekeza dawa fulani. Hivyo, hata Maswahaba wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) walitambua hakika sababu na hekima zilizomo ndani ya maamuzi yake.
Ama kwa Ijtihaad…
Maelekezo ya kwamba Ijtihaad inaruhusika na inafaa kwa matumizi ya misamiati ya leo ni mengi. Kwa mfano, Mu’adh bin Jabal (Radhiya Allaahu ‘anhu) anaeleza kwamba wakati Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipompeleka
“Utafanya nini
Ijtihaad hii na kutumia hukumu yake mtu mwenyewe
“Hakikisha unaelewa vizuri kila kesi ambayo imeletwa kwako ambayo hamna maandiko yanayohusiana nayo kutoka kwenye Qur-aan au Sunnah. Kwako, baadaye, ni jukumu la kuoanisha na kufananisha, ili kutofautisha mifano kwa lengo la kufikia hukumu ambayo ipo karibu na uadilifu na bora mbele ya Allaah[9].”
Hapo hapo, al-Imaam ash-Shafi’iy ameeleza “rai”
Abu Bakr asw-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ‘anhu), Khaliyfat Rasuul Allaah, amesema: “Namna Mtume alivyo, rai zake daima zilikuwa ni sahihi kwa sababu Allaah daima Akimuongoza. Ama katika kesi yetu, tunadhania na tunakisia.[11]”
Hivyo, tunaweza kusema kwamba dhana ya Ijtihaad au “rai”, kwenye kipindi hicho, haikwenda mbali zaidi ya moja zifuatazo:
a) Kutumia maana moja au nyingine zinazowezekana katika kesi ambapo hukumu inaweza kujikubali yenyewe katika tafsiri zaidi ya moja. Mfano, pale Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipowaamrisha Waislamu kuswali sehemu ya Banu Quraydhwah[12].
b) Mlinganyo, Qiyaas, ambayo inahusu suala kwa kulifananisha na jengine, pia suala
c) Ijtihaad ya kutia maanani kitu ambacho kinawezekana kuwa na manufaa au kuzuia kitu ambacho kinaweza kupelekea kwenye ubaya, au kuchukua uamuzi fulani kutoka kwenye matamko ya jumla, au kutumia tafsiri maalum, na mengineyo zaidi.
Bidii ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwahamasisha Maswahaba kufanya Ijtihaad na kuwafundisha katika matumizi yake inaweza kuonekana kwenye maneno ya Hadiyth hii:
“Hakimu anapofanya Ijtihaad na kufikia kwenye hukumu sahihi, anapata ujira mara mbili, na kama hitimisho lake si sahihi, pia anapata ujira mmoja.[14]”
Ijtihaad ya Maswahaba wengi ilikuwa ni makini na kwamba kwenye kesi nyingi, uteremsho wa Qur-aan ulihakikisha huo umakini. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliikubali. Bila ya shaka, ukaribu wao na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ulitosheleza wepesi wa kutambua malengo ya Mwingi wa Busara na Mtunga sheria, madhumuni makuu yaliyo ndani ya Sheria za Qur-aan, na maana ya maandiko. Nafasi ambayo waliokuja baada
[1] Angalia ‘Abdullaah Ibn ‘Abdur-Rahmaan ad-Daarimiy, Sunan, I,
[2] Ad-Daarimiy, Sunan, I,
[3] Ad-Daarimiy, Sunan, I,
[4] Ad-Daarimiy, Sunan, I,
[5] Ad-Daarimiy, Sunan, I,
[6] Imenukuliwa na Shaykh ‘Aliy Abdur-Razzaq ndani ya Tamhiyd li Taariykh al-Falsafah,
[7] Ad-Dahlawiy: HujajatuLlaah al-Baalighah, (Misri), I,
[8] Kwa maelezo kuhusiana na usahihi wa kunukuu Hadiyth
[9] Angalia Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqi’iyn
[10] Angalia al Imam ash-Shaafi’iy, Ar-Risaalah, (
[11] Ibn Qayyim, I’laam al-Muwaqqi’iyn, I,
[12] Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaamrisha kundi la Waislamu pamoja na maelekezo: “Simamisheni Swalah ya Laasiri sehemu ya Banu Quraydhwah.” Wakitoa tafsiri
[13] Hadiyth ni maarufu na ni sahihi, na iliingizwa ndani ya vitabu vya Imaam al-Bukhaariy, Abu Dawud, al-Nasaaiy, Ibn Maajah, na Ahmad katika mkusanyiko wa Hadiyth.
[14] Hadiyth hii ni ya maana na ilipokewa na al-Bukhaariy, Muslim, na wengineo katika mkusanyiko wao wa Hadiyth sahihi.