13-Uswuul Al-Fiqhi: Wakati Wa ‘Uthmaan Ibn ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘anhu)

 

‘Uthmaan alipopatiwa utii, alifanya kwa misingi wa kwamba anafanya kazi kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah, Sunnah ya Mtume Wake, na kufuata maamuzi yaliowahi kutolewa na Makhalifa wawili. Hili, aliweka ahadi kulitimiza. Hata hivyo, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha kwamba atakapokuwa Khaliyfah, atajitayarisha kufanya kazi kwa mujibu wa Kitabu cha Allaah na Sunnah ya Mtume Wake, na kisha kutumia jitihada zake za mwisho na nguvu atakayoweza katika elimu yake. Kwa sababu ‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alionesha kwamba alikuwa tayari kuichukua kazi kulingana na sheria zilizowekwa na Makhalifa wawili wa mwanzo, aliungwa mkono na ‘Abdur- Rahmaan, ambaye alikuwa na maamuzi ya mwisho. Hivyo, chanzo cha tatu cha sheria, maamuzi yaliyotolewa na Makhalifa wawili wa mwanzo ilijumuishwa wakati wa Khaliyfah wa tatu, na yeye alikubali.

 

Kwa kuwa ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa na nafasi yake kuhusiana na hili, pale yeye mwenyewe alipokuwa Khaliyfah alifanya kazi kwa mujibu wa Ijtihaad yake mwenyewe katika masuala ambayo Khulafaa’ waliopita tayari walikuwa washatoa Ijtihaad. Kwa mfano, ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alifanyia kazi kwa mara nyengine suala la aidha mtumwa wa kike aliyepata watoto kwa bwana wao anaweza kuuzwa.

 

‘Uthmaan ibn ‘Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alikuwa mmoja kati ya Swahaabah ambaye hakutoa idadi nyingi za Fatawa, labda kwa sababu masuala ya msingi aliyokutana nayo, yalikuwa tayari yameshafanyiwa kazi na Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhum), na alipendelea kutumia maoni yao. Lakini kwa kesi nyingine, alilazimika kufanya Ijtihaad, kama walivofanya waliomtangulia. Mara moja, kabla ya ‘Uthmaan kuwa ni Khaliyfah, ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alimuuliza kuhusiana na suala la kisheria. Akijibu, ‘Uthmaan alisema: Kama utafuata maoni yako mwenyewe, hivyo itakuwa ni sahihi. Lakini, kama utafuata moni ya Khaliyfah kabla yake (yaani Abu Bakr), ni bora, kwa sababu alikuwa ni mzuri sana katika kutoa maamuzi.”

 

Pia alitekeleza Ijtihaad yake mwenyewe, wakati wa Hajj, hakupunguza Swalaah sehemu ya Minaa ingawa inaruhusika kufanya hivyo. Kuna ufafanuzi wa aina mbili kuhusiana na hili: ya mwanzo ni kwamba ameoa Makkah, na akafikiri kwamba watu wa Makkah hawaruhusiki kupunguza Swalaah hapo Minaa, ufafanuzi wa pili ni kwamba alikhofu kwamba Mabedui wataingiwa na wasiwasi pale watakapomuangalia yeye akifanya hivyo, na hivyo hakufanya.

 

‘Uthmaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) pia alitengeneza Ijtihaad kwamba watu wote wasome Qur-aan kwa mujibu wa mtindo wa kisomo cha Zayd (Radhiya Allaahu ‘Anhu), kwasababu aliona kwamba hii ilikuwa ni sauti iliyo bora, na inayowezekana kuwa ni bora katika kuzuia kutokezea kwa migongano.

 

 

Share