Sharbati ya Peya (Avocado Shake)
Sharbati ya Peya (Avocado Shake)
Vipimo
Peya - 2
Maziwa - 4 gilasi
Maji - 1 gilasi
Sukari - kiasi
Lozi - 1/4 kikombe
Namna ya Kutayarisha:
- Menya peya, toa kokwa.
- Roweka Lozi kisha umenye maganda na ukate kate ndogo ndogo au tumia za tayari.
- Tia peya, maziwa na sukari katika mashine ya kusagia (blender) na vipande vya barafu kidogo usage.
- Ikiwa nzito bado ongeza maji
- Mimina katika gilasi, pambia lozi.
