05-Fatwa: Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr
Kuwakilisha Katika Kulipa Zakaatul-Fitwr
SWALI:
Baadhi ya miskiti wanaashiria kupokea kiwango cha Zakaatul-Fitwr kutoka kwa watu ili wagawe kwa wanaohitaji kwa ajili yao. Hugawa chakula kama mchele, unga n.k. Je, desturi hii ni sawa?
JIBU:
AlhamduliLLaah
Kwa vile imekusudiwa kununua na kugawa bidhaa kwa wanaohitaji (hizo bidhaa) kwa ajili yao, hivya ni sawa na watapa thawabu In Shaa Allaah.
Na Allaah Anajua zaidi