04-Fatwa: Zakaatul-Fitwr Ni Chakula, Si Pesa Na Itolewe Kwa Waislamu Wanaohitaji Pekee

 

Zakaatul-Fitwr Ni Chakula, Si Pesa Na Itolewe Kwa Waislamu Wanaohitaji Pekee

 

 

 www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Kitu gani unatoa kwa ajili ya Zakaatul-Fitwr? Ni pesa au chakula. Vipi ikiwa humjui mtu wa kumpa? Je, inaruhusiwa kuitoa katika miskitii au kwa kafiri asiye na mahali pa kuishi au kafiri kwa ujumla?

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah

 

Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliifanya kutoa swaa' (pishi) ya tende au swaa' ya shayiri kuwa ni Zakaatul-Fitwr iliyowajibika kwa Waislamu wote, mtumwa aliye huru, mwanamke na mwanamume, kijana na mzee, na akaamrisha kwamba itolewe kabla ya watu kwenda kuswali (Swalaatul-'Iyd). [Al-Bukhaariy]

 

Abuu Sa'iydil-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Tulikuwa tukilipa Zakaatul-Fitwr swaa' (pishi) moja ya chakula, au swaa'  ya shayiri (ambacho ndicho kilichokuwa chakula chao zama hizo) au swaa'  ya tende au swaa' ya aqitw (mtindi mkavu) au swaa'  ya zabibu" [Al-Bukhaariy]

 

Kwa dalili hizo, ni dhahiri kwamba Zakaatul-Fitwr lazima iwe ni chakula, si pesa. Hivyo lazima tutekeleze ilivyoamrishwa katika Sunnah. Hivyo lipa swaa' moja ya chakula chochote kinachotumika na watu katika nchi yako mfano mchele au ngano kwa ajili yako na kila mtu katika nyumba yako. (swaa' (pishi) ni sawa na taqriban Kilo 2 12 au 3). 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share