Zakaah Ya Mkopo Wa Mali Inayofanyiwa Biashara

SWALI:

 

 

Ama baada ya salamu natoa shukrani zangu zisizo kifani kwa kuwepo kwa mtandao huu, M/Mungu atujaalie uendele kuwepo na utanuke zaidi na zaidi, Amin. 

 

 

swali langu ni moja ama mawili, nimeshasoma katika masuala ya zakka kiasi kinachoweza kufikiwa ili mtu atoe lakini maelezo yanasema 2.5% itolewe kutoka katika 82.5g ya dhahabu ama pesa yenye thamani sawa na hiyo.

 

 

swali ni...mama yangu ana milioni

 

ekopa ili afanye biashara na analipa marejesho kwa hao wakopeshaji, faida kwa mwaka mzima inawez kuwa milioni 4 mpaka 6 kwa mwaka mzima na faida hiyo hiyo ndiyo anatumia kusomeshea watoto, yaani hana msaada kutoka kwa mzee wangu, je anatakiwa kulipa zakka? na kama ndiyo atalipa vipi zakka? Naomba mahesabu ya kukokotoa ili ajue anatakiwa kutoa kiasi gani.

 

 

Halafu nakuomba unipe thamani ya 1 g ya dhahabu katika Tsh/

 

 

Assalam alaykum.   

 


 

 

 

JIBU:

 

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola  wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani zetu za dhati kwa ndugu muulizaji swali. Mwanzo ni masikitiko makubwa kuona kuwa mama ndiye mwenye kwenda mbio katika kuhakikisha kuwa watoto wamesoma na mzee mbali na kuwa hukutoa udhuru ni kwa nini hatekelezi jukumu

 

lake hilo. Majukumu yote kuanzia kumwangilia mkewe na watoto ni la baba mzazi na ni juu kufanya juhudi kutekeleza hayo. Ikiwa ana udhuru basi tunamuomba Allaah Aliyetukuka Amsahilishie hayo. Au kama wameachana, basi tunamuombea mama huyo usahali na tawfiki ya kuwezeshwa yote hayo na Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala).

 

 

Ama tukiingia katika suala lako tungependa kusema yafuatayo:

 

 

 

Mwanzo wa yote ni kuwa si wote wenye kujibu maswali wanatoka

 

Tanzania hivyo kwa kuwa una watu huko inabidi nawe ufanye juhudi ya kuulizia bei ya gramu 1 ya dhahabu swafi (yaani krat 24). Na fahamu kuwa bei hiyo huwa inabadilika mara kwa mara, hivyo, ni bora uulizie kwa wakati ule unaotaka kutoa hiyo Zakaah.

 

 

Ama kuhusu mtaji wa biashara ambao mamako alikopa ni kuwa faida pekee ndiyo itakayoingia katika mahesabu ya Zakaah. Katika hayo uliyotuelezea ni kuwa mdaiwa anafaa yeye ndiye asaidiwe na pesa za Zakaah hivyo yeye hawajibiki kutoa kwani Allaah Aliyetukuka Anatuambia: “Na wenye madeni” (9: 60). Ikiwa mama labda anaona hata hivyo anataka kusaidia wengine kwa kipato anachopata basi hapo ndio tunaweza kufanya mahesabu.

 

 

 

Kwa hali yoyote ile atakuwa ameandikiana na anayemdai jinsi ya kulipa deni

 

lake hilo. Tuchukue kuwa kila mwaka anafaa alipe milioni mbili kupunguza deni lake. Baki ya faida ni milioni 4 ikiwa atapata faida kubwa kabisa. Kutokana na faida hii anafaa alipe masurufu ya chakula, karo za shule, nguo, matibabu, ijara ya nyumba pengine na masurufu mengineyo yote yatatolewa kutoka kwa faida. Sasa ile faida iliyobaki ikiwa imefika kiwango hicho cha chini ambayo kwa mahesabu hayo ya kupachika itakuwa (82.5 X 26250 (makisio ya bei ya gramu moja ya dhahabu Tz) = Tsh. 2,165,625). Kwa hiyo, ukiwa na pesa hiyo kisha ipitiwe na mwaka wa Kiislam katika hali ya kutopungua ndio itabidi aitolee Zakaah. Hiyo ikiwa kama atakuwa na pesa hiyo ukitazama kama ulivyotueleza kuwa ana majukumu mengi.

 

 

Huko ni kwenda mbali tu lakini inafaa yeye amalize deni

 

lake mwanzo kisha ndio awe ni mwenye kuingia katika watoaji Zakaah akiwa na kiwango hicho.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 


Share