Kuswali Swalah Ya Safari Kwa Sababu Ya Udereva
SWALI:
Mimi nafanya kazi ya udereva hapa ulaya wa kuendesha basi la abiria wa town bus (DALADALA). Swala langu ni kwamba INAFAAA KWA mimi kuswali safari??? kwa sababu time nyingine ninakua sipati nafasi kwa sababu ukianza unakua unaenda kwa timu hadi unamaliza sasa time nyingine unachelewa hata timu ya kujinyoosha hamna yaani ukiingia kwenye usukani hadi 4 hrs later ndio unapata nafasi ya kutoka, au sipati maji ya kutia udhu au sehemu yenyewe inakua haisihi kuswali je inafaa kwa mimi kuswali safari?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani ndugu yetu kwa swali lako
Mwanzo hukutuambia uendeshaji wako wa daladala unakuwa kutoka wapi hadi sehemu gani. Je,
Ama katika kadhia yako ikiwa uko mjini, basi unaweza baadhi ya nyakati kwa dharura hizo, kuunganisha Swalah mbili kwa pamoja, yaani Adhuhuri na Alasiri, au Magharibi na 'Ishaa lakini kwa kuziswali zote kamili na si kwa kuzifupisha. Ila usilifanye
Hakika wakati ni mtu kujipanga kwani hakuna uzito aina yoyote. Ikiwa una hima ya kweli unaweza hata kuzungumza na waajiri wako wakuweke ile zamu ya asubuhi ambayo itakupatia wewe fursa ya kuweza kutekeleza jukumu la Swalah kwa wakati wake. Inabidi uwaelezee waajiri umuhimu huo ili waweze kuelewa. Ikiwa wameelewa utapata afueni kubwa lakini usikae tu bila kujieleza ni lazima ufanye juhudi katika
Sijui hayo masaa bayo unasema unafanya mfululizo huwa ni namna gani? Je, unapoanza huwa hakuna hata ile nafasi ya kwenda chooni kujisaidia au kufika kituo na kubeba watu kwa dakika chache au ni vipi? Ikiwa zipo hizo nyakati basi hakutakuwa na shida yoyote kwani unaweza kutumia fursa hiyo.
Ama hakika kuswali si lazima maji yapatikane. Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameifanya Swalah kuwa ni nguzo isiyokuwa na udhuru wa aina yoyote. Muislamu akikosa maji basi ameruhusiwa na sheria kutumia mchanga ili afanye tayamamu. Hivyo, ikiwa maji hakuna utatumia vumbi au mchanga kwa ajili ya kushika wudhuu na kisha kuswali.
Lakini tunayofahamu
Ama sehemu kutosihi haipo katika Uislamu kwani ardhi yote imejaaliwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kuwa ni twahara. Kwa hiyo, Muislamu akifikiwa na wakati wa Swalah anaweza kuswali popote ila tu ikiwa ataona najisi ya dhahiri. Hivyo usitie wasiwasi kabisa kuhusu sehemu ya kuswalia.
Na pia kuna uwezekano wa kuchukua wudhuu katika maeneo vilivyopo vyoo huko kwenye vituo vya ma-bus au daladala kwa inavyojulikana, na hata humo mnapoanzia kuchukua daladala. La kufanya ni kuingia na kikombe chako cha kutumia na kutupa 'disposable cups' na kutumia kuwekea maji na kujisafisha nayo baada ya kujisadia, kisha ukaenda kuchukua wudhuu kwenye beseni (sink) zilizopo nje ya vyoo na ukifika sehemu ya miguu na ikiwa unachelea kuweka miguu yako kwenye hizo beseni kwa kuwa utawakera wengine ambao si Waislam, unaweza kupaka maji juu ya viatu vyako au soksi zako na ukaswali nazo, kwa sharti tu uhakikishe kuwa ulishanuia kufanya hivyo na kuchukua wudhuu wote na miguu kabla hujaamua kupangusa hivyo viatu au soksi baadaye (unaweza kuchukulia huo wudhuu kamili nyumbani kabla hujatoka, kisha baadaye utakuwa unapungusa tu juu ya viatu au soksi ukiwa uko kazini au njiani).
Soma Swali katika kifungo kifuatacho upate maelezo ya kuchukua wudhuu huo unaoitwa mashul-kufayn (kupangusa juu ya soksi/viatu):
Mtu Mgonjwa (Kilema) Afanye Wudhuu Vipi Na Aswali Vipi?
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Akufanyie sahali suala lako
Na Allaah Anajua zaidi