Mgonjwa Kupunguza Swalah Na Kuziunganisha

SWALI:

ASSALAMU ALAYKUM  

Mama yangu ni mgonjwa hivyo husali kama msafiri yaani kuakhirisha au kutanguliza pamoja na kupunguza rakaa [kila sala ya rakaa nne kusali mbili]. Naomba  ufafanuzi.

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa muulizaji na tunamuomba Allaah Aliyetukuka Akuafu na kumponyesha mamako arudi katika hali yake ya awali

Ama kuhusu swali lako ni kuwa Uislamu umekuja na Sharia ya tahfifu na usahali katika mipaka iliyowekwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo, mambo yetu yote ni lazima yaende sambamba na muongozo waliotupatia wao.

Katika suala la kupunguza Swalah ni wakati wa safari ambako kumeidhinishwa na Sharia, ama katika hali ya ugonjwa akiwa mgonjwa ana taklifu basi anaweza kuunganisha Swalah lakini sio kupunguza. Kwa ajili hiyo inatakiwa umueleweshe mamako kuhusu hilo. Na kule kupunguza kwake kwa kutokujua atakuwa ni mwenye kusamehewa na Allaah Aliyetukuka.

Kwa Maelezo zaidi somo Maswali na Majibu yanayohusu maudhui hii katika viungo vifuatavyo: 

Swalah Ya Mgonjwa

Mtu Mgonjwa (Kilema) Afanye Wudhuu Vipi Na Aswali Vipi?

Swalah Ya Mgonjwa Anayeswali Kwa Kuketi Akiwa Kavaa Viatu Inafaa?

Tunarudia tena du’aa yetu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Amsahilishie mamako ugonjwa wake na iwe ni kafara ya kufutiwa madhambi kwa hilo.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share