Kwa Nini Watoto Wa Nabii Ibrahiym Tofauti Kwa Ukabila?
SWALI:
assalamu alaykum ningependa kujua kwamba kwanini watoto wa nabii ibrahim ni tofauti mmoja ni baba wa waarabu na mwengine ni baba wa majushi sasa ningependa munifahamishe kwanini iwe hivyo assalamu alykum
JIBU:
AlhamduliLLaah - Sifa njema zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwako ewe ndugu yetu kwa swali lako zuri. Bila shaka inaeleweka kuwa sote (wanaadamu) tu ndugu katika ubinadamu kwani baba yetu ni mmoja. Kwa uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Akatujaalia kuongozeka kwa kiasi kikubwa
Kwa uwezo Wake pia Akatufanya kutoka na mwanamme mmoja na mwanamke mmoja kuwa mataifa na makabila tofauti ili tupate kujuana wala sio kukejeliana (49: 13). Tunaweza kujiuliza vipi sote tumetokana na Nabii Aadam (‘Alayhis Salaam) na mkewe Hawwaa na sasa tumekuwa watu wa makabila na lugha tofauti? Kwa nini tusiwe wa kabila moja? Jawabu la hii ni ile kauli ya Allaah Aliyetukuka: “Na katika Ishara Zake (za kuonyesha uweza Wake) ni kuumba mbingu na ardhi, na kuhitilafiana ligha na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo Ishara kwa wenye ujuzi” (30: 22).
Na kutuonyesha uwezo Wake (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema: “Lau Angependa Mola Wako Angewajaalia watu wote kuwa Ummah mmoja lakini wanaendelea kutofautiana” (11: 118).
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Alimpatia mwanaadamu ufahamu na elimu ya vitu vyote kwa kuweza kuvipatia majina ili kwayo aweze kufundisha wengine na kutoa majina kwa vinavyokuja baadaye. Kwa njia hii wanaadamu wakaweza kwa kila kizazi kilipokuwa kinazaana kujipatia jina la familia hiyo.
Tukija kwa Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) inaeleweka kuwa alikuwa na wake wawili ambao kwao alipata watoto wawili waliopata umaarufu na kuchaguliwa kuwa ni Manabii – Ismaa‘iyl na Is-haaq (‘Alayhimas Salaam). Kwa vile aliye mkubwa alipelekwa na kukulia katika wangwa wa Makkah ulio
Tukichukua mtoto wa Nabii Ibraahiym, yaani Is-haaq (‘Alayhis Salaam) jina
Kwa ufupi hapana tatizo katika
Na Allaah Anajua zaidi