Kujipaka Cream Kwa Ajili Ya Kuung’arisha Uso

 

Kujipaka Cream Kwa Ajili Ya Kuung’arisha Uso

 

Alhidaaya.com

 

 

Swali:

 

Mimi nimeolewa na nina watoto watano, nataka kujua kama niko kwenye dhambi au la kwani ni bora mwanadamu kufanya mambo ambayo Allaah anayapenda, Alhamdulillah naswali na kufuata mwanamke jinsi anavyotakiwa.

 

Swali langu mimi mwili wangu mikononi, miguuni ni meupe, lakini uso ndio umefifia na nikiacha kutumia cream naharibika sana uso. Sasa natumia cream ambayo sio mkorogo yaani nakuwa nangaa usoni na ninataka nimpendezeshe mme wangu.

 

Nitafahamu kufahamu sisi kama wanawake Waislam lazima tuwe na mifano mizuri

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho 

 

 

Hakika ni kuwa Uislamu unamtaka mume na mke warembesheane ili ule upendo na mahaba yaingie kwa kila mmoja wao kwa mwengine. Kutumia cream kwa ajili ya kuurembesha uso ikiwa hautakuwa ni wenye kuonekana hayo na mwanamme mwingine ambaye si maharimu wako hakuna tatizo lolote. Na ikiwa cream itakuwa ni dawa kwa tatizo ulilo nalo la ngozi basi haikatazwi kutumia. Muhimu isiwe ni cream yenye madhara kwa mwili au yenye kubadilisha rangi ya mwili au maumbile kwa ujumla.

 

 

Nasaha ambayo tunaweza kukupatia ni kuwa ni bora kwako uende kwa mtaalamu akiwa ni Muislamu ni vyema zaidi ili aweze kukushauri juu ya cream inayofaa kuitumia. Tuelewe kuwa cream inatengenezwa kwa kutimia makemikali hivyo ikiwa itakuwa ni yenye kukuletea madhara utakuwa hufai kuitumia. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘aalaa): Anasema:

 

وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ.

Wala msijitupe katika maangamizi... [Al-Baqarah: 195]

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share