Daku: Ufafanuzi Wa Wakati Wa Mwisho Wa Kula Daku
SWALI:
Kuhusu kula daku, hapo naomba ufafanuzi hasa maana huku sisi hatuswali Alfajir twaswali Assubhi, sasa tukiwaruhusu watu kula mpaka wakati wa adhana ya mwisho mi nahisi tutakuwa tushawalisha watu mchana. Wajua hawa watu wanaoandaa nyakat za swala wao wenyewe wanasema tufanye makadirio ya nyakati swala. Naomba unifafanue pia hapo.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako la nne. Kuhusu ufafanuzi wa swali la:
Ndugu kwa wakati huu wetu wa sasa tunafaa tusiwe na utata wowote kwani waliotutangulia wlifanya bidii kwa kufanya utafiti hadi wakatuwekea jedwali ya machomozo ya jua na machweo yake.
Ni vizuri kuwa na jedwali ya mwaka mzima na kutazama wakati wa kuingia Alfajiri ya kweli ambao ndio wakati wa uhakika wa adhana ya pili. Katika kipindi cha hasa Ramadhaan maratibu wa Msikiti wenu mzungumze na kamati au Imaam aelezwe mwadhini wakati wenyewe na hapo hakutakuwa na utata wowote. Labda tukitoa mfano itaeleweka zaidi nayo tukichukua wakati wa adhana ya pili na machweo kwa mji wa
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anasema kuhusu nyakati hizo:
“Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku” (2: 187)
Lakini kama tulivyosema hapo juu ni kuwa tatizo hili linafaa lisiwepo kwa ajili ya juhudi zilizofanywa kuhusu suala
Na Allaah Anajua zaidi