Kumkaribisha Mgeni Kinywaji Katika Ramadhaan

SWALI:

ASSALAM ALEIKUM

JEE YAFAA KUMKARIBISHA MGENI KINYWAJI SIKU YA RAMADHAAN?

 





 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Shukrani ndugu yetu kwa swali lako. Kuhusu hilo linategemea na ugeni wa huyo mtu. Hakika ni kuwa wapo watu kama makafiri hawafungi na hata wakifunga basi funga yao haichukuliwi kabisa. Na wengine ni watu wenye udhuru kama mwanamke mwenye nifasi, hedhi, mimba na mwenye kunyonyesha, pia msafiri, mgonjwa na mkongwe asiyeweza kufunga kabisa. Hawa wote wameruhusiwa na sheria hivyo mgeni akiwa ni mwenye udhuru wa kisheria ni wajibu wake kula akiwa hakufunga. Watu kama hawa unaweza kuwapatia chakula.

 

Ama mgeni ambaye ni Muislamu, aliye baleghe, muweza, mkaazi na mwenye akili timamu lakini anataka kukirimiwa bila udhuru wowote, huyo haifai kumkaribisha kwa chochote kile. Na ikiwa utamkaribisha basi utakuwa ni mwenye kupata dhambi kwani utakuwa ni mwenye kumsaidia mtu katika jambo la dhambi.

 

Na Allaah Anajua zaidi'

  

Share