Wanaume Kula Zaafarani Inaruhusiwa?
SWALI:
ningependa kuuliza wanaume hawafai kula zaafarani?siku zote nijuavyo haina neno hutia kwa chakula,nimeskia hivi juzi ya kuwa kiislaam hairuhusiwi. Tafadhali nijulisheni ikiwa ni ukweli na kwa sababu gani.
Shukran kwa jitihada zenu kutuongoza. Mungu awajaze kheyr. Ameen
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Kuhusu suala
Bila shaka ikiwa inatolewa Zakaah itakuwa kuliwa pia hakuna tatizo kwa wanawake na wanaume.
Ama ikiwa unataka kujua kama inafaa kunywewa kama wanavyofanya wale wanaotengenezewa na waganga au mashekhe wa uongo kuwa ni kama dawa au kinga na kuandikiwa maandishi ya Qur-aan kwenye sahani kasha ikachanganywa na maji kisha akapewa mtu anywe, basi hiyo haifai na si sawa mtu kutumia. Haifai kutumia si kwa sababu ya zaafarani, bali ni kwa sababu njia hiyo iliyotumika si ya kisheria ambayo ni njia ya udanganyifu unaotumiwa na watu kwa kutumia maneno ya Allaah na kuvumbua mbinu mbalimbali za kutafutia chumo ndani yake kwa njia za udanganyifu kama hizo za kutengeneza kombe kwa Qur-aan, maji na zaafarani. Jambo
Na Allaah Anajua zaidi