21-Uswuul Al-Fiqhi: Majukumu Ya Wafuasi Wa Abuu Haniyfah Katika Uandishi Wa Al-Uswuul
MAJUKUMU YA WAFUASI WA ABUU HANIYFAH KATIKA UANDISHI WA AL-USWUUL.
Baadhi ya Wanahistoria wa Uswuul al-Fiqhi wametoa maoni kwamba al-Qaadhi Abuu Yuusuf na Muhammad bin al-Hassan wameandika kuhusu Maarifa ya Sheria za Kiislamu,[64]lakini dai hili halijathibitishwa.
Mwandishi wa Kashf adh-Dhwunuun[65] amenukuu ‘Ala’ pamoja na misemo ya ‘Ala’ ad-Diyn kutoka Mizaan al-Uswuul “Mizani ya Uswuul.”
Tambua ya kwamba Uswuul al-Fiqhi ni tawi la Uswuul ad-Diyn na kwamba utungaji wa kitabu chochote ni lazima uwe umeathirika na imani za mwandishi. Hivyo, kwa vile wengi wa waandishi wa Uswuul al-Fiqhi wametokana na Mu’tazilah wenye kutofautiana na sisi kwenye kanuni kuu, au kwa Ahl al-Hadiyth wenye kutofautiana na sisi kwenye masuala ya kina, hatuwezi kutegemea vitabu vyao.
Vitabu vya Wanazuoni wetu (wa Hanafi), hata hivyo, ni vya aina mbili. Aina ya mwanzo ni vile vitabu vilivyoandikwa kwa mtindo makini kabisa, kwa sababu waandishi wao walijua vyote viwili; kanuni na matumizi yake. Mifano ya aina hii, ni: Ma’khaadh ash-Shar’iy “Kuiendea Sharia’h” na al-Jidaal “Mjadala”” vilivyoandikwa na Abuu Mansuur al-Maturidi (Amefariki mwaka 333 H.).
“Aina ya pili ni ya kitabu kilichojadili kwa umakini kabisa pamoja na maana ya maneno na yaliyopangwa vizuri, kwa kuegemea mantiki za waandishi wao kwa kufikia suluhisho zenye maelezo kutokana na maana dhahiri za usimulizi. Hata hivyo, hawakuwa mahiri katika kushughulikia na nukta nzuri za al-Uswuul au masuala ya hoja safi. Matokeo ni kwamba waandishi wa aina ya pili walitoa mawazo kwenye kesi ambazo walikubaliana na wale waliopingana. Juu ya hivyo, vitabu vya aina ya mwanzo vilipoteza hadhi, ama kwa sababu vilikuwa ni vigumu kuvielewa au kwa sababu wanazuoni walikosa taratibu muafaka za kufanya kazi hii.”
Kuna mengi ambayo yanaweza kusemwa kuhusu usahihi wa tamko hili unavyofafanua maendeleo ya masomo ya Hanafi kwenye al-Uswuul, hata kama ilifanywa na mwanazuoni wa Kihanafi. Tamko hili, halifanyi lolote, kufikia karibu na ukweli wa kuelezea jukumu la Hanafiyyah kwenye maendeleo ya Uswuul al-Fiqhi. Kwenye kipindi cha mwanzo, wanazuoni hawa walijishughulisha zaidi kwenye kujadili masuala yaliyoletwa juu na al-Imaam ash-Shaafi’iy ndani ya ar-Risaalah yake kuliko kabla ya al-Imaam al-Maturdi, kama alivyofanya ‘Iysa bin Abbaan na wengine.
Wakati wa kipindi kinachofuata, mmoja miongoni mwao (ambaye) ni mwandishi mkubwa wa al-Uswuul alikuwa ni Abuu al-Hassan al-Karkhi (Amefariki mwaka 340 H). Kitabu chake kwenye al-Uswuul kinahusisha idadi maalum ya kurasa ambazo zilichapishwa na kitabu cha Abuu Zayd ad-Dabuzi, Ta’siys an-Nadhwar “Kuanzisha Maoni”, ambacho kimechapishwa ndani ya matoleo kadhaa nchini Cairo.
Baadaye, Abuu Bakr al-Jassaas (Amefariki mwaka 370 H.) aliandika kitabu chake, Al-Fuswuul Fiy al-Uswuul kama ni utangulizi wa kitabu chake Ahkaam al-Qur-aan “Tafsiri za Kisheria za Qur-aan”.[66]Al-Fuswuul kimechunguzwa na kufanyiwa uhariri kwa ajili ya uchunguzi wa shahada ya tatu (doctoral thesis), na kilichapishwa hivi karibuni nchini Kuwait.
Maendeleo ya kweli ya maandiko ya ki-Hanafi kwenye somo la al-Uswuul, inawezekana kutambulika kuanza kwa al-Imaam Abuu Zayd ad-Dabuuzi (Amefariki mwaka 340) ambaye aliandika vitabu viwili muhimu kwenye mada. Taqwiym al-Adillah “Thamani ya Ushahidi”, vyote au baadhi yake ambavyo vimechunguzwa na kuhaririwa, lakini bado havijachapishwa, na Ta’siys an-Nadhwar[67]Abuu Zayd aliifanyia kazi vyema al-Uswuul (kama) walivyofanya waliomtangulia, haswa kwa Al-Karkhi na Al-Jassaas, lakini kwa tofauti ambazo aliupanua uwanja na kuuelezea kwenye maelezo ya kina zaidi, pia alifanya nukuu fupi fupi kwenye nukta ambazo Hanafiyyah (Mahanafi) walikubalina na kutokubaliana na wengine, kwenye masuala ya Uswuul.
Abuu Zayd alifuatwa na Fakhr al-Islaam al-Baydaan (Amefariki mwaka 482 H.) ambaye ameandika kitabu maarufu cha Kanz al-Wuswuul Ilaa Ma’rifat al-Uswuul “Hazina ya Kuifikia Elimu ya Uswuul”, ambacho alijadili kuhusu Uswuul kwa jumla. Baadaye wanazuoni wa Hanafiyyah waliangalia kwa faida kubwa kwenye kitabu hicho na kuandika fafanuzi nyingi kwenye hicho kitabu, kilicho bora na muhimu zaidi, kilikuwa Kashf al-Asraar “Siri Zimefichuliwa” na ‘Abd al-Aziyz al-Bukhaariy (Amefariki mwaka 830). Fafanuzi hii imechapishwa kwenye matoleo kadhaa yaliyofanyiwa uhariri kote kuwili, huko nchini Uturuki na Misr.
Vivyo hivyo, Shams al-Aimmah as-Sarkhaasiy (Amefariki mwaka 423 H) ameandika Uswuul as-Sarkhaasiy, ambacho kimechapishwa ndani ya juzuu mbili nchini Misr. Kitabu hichi kinatambulika kuwa; kwa njia zote (kama ni) kitabu mbadala kwa kusoma kitabu cha Daabusi Taqwiym al-‘Adillah. Wanazuoni wa Hanafiyyah wa al-Uswuul wamechukua juhudi kubwa binafsi kwenye vitabu vya al-Bazdaawiy na as-Sarkhaasiy na wakajihusisha wenyewe kwenye kuvisomesha na kuvifafanua kwa muda mrefu.
Kutokana na hapo juu, ieleweke wazi kwamba maendeleo ya Uswuul al-Fiqhi, kama ni somo linalojitegemea, limekamilika, na kwamba hoja zake na mipaka ya elimu (parameter) zimetolewa tafsiri kwenye Karne ya tano AH. Hakika, kwa karne hiyo wanazuoni wa kila mafunzo ya fikra za kisheria wamerikodi tafsiri zao wenyewe na ufahamu wa Uswuul al-Fiqhi.
MTINDO WA WAFUASI WA AL-IMAAM ASH-SHAAFI’IY AU “MUTAKALLIMUUN”, NA WALE WA HANAFIYYAH (KI-HANAFI).
Uandishi wa somo la al-Uswuul, kiujumla unafuatiwa moja kati ya mitindo ifuatayo. Wa kwanza ulikuwa ni mtindo wa ash-Shaafi’iy au mtindo wa Mutakallimuun. Huu ulikuwa mtindo uliofuatwa na Shafi’iyyah, Malikiyyah, Hanaabilah na Mu’tazilah,[68]na ilitambuliwa kama ni “Mtindo wa Mutakallimuun” kwa sababu waandishi wa vitabu vilivyoandikwa kwa mujibu wa mtindo huu, walizoea kuzitolea utangulizi pamoja na mijadala ya elimu ya sifa za Uislamu na masuala thabiti, kama vile al-Hasan na al-Qabiyh “Nzuri na mbaya”, Hukm al-Ashyaa Qabl ash-Shar’iy “Hukmu Ya Masuala Kabla Ya Kuteremshwa Shari’ah”, Shukr al-Mun’im “Haja ya Shukrani Mtoaji”, na al-Haakim “Mmiliki wa Mamlaka” Sababu nyengine ya kubandikiwa “Mtindo wa Mutakallimuun” ni kwa matumizi ya mtindo wa kudhihirisha kwenye kutafsiri misingi ya utaratibu wa chanzo, kwenye kuangalia uhalali wa misingi hiyo, na katika kuzibatilisha kwa wale wenye mawazo yaliyotofautiana bila ya kutilia mkazo kwenye masuala na maelezo yenye kutokana na mzizi wa matumizi ya misingi hii.
MTINDO WA WANAZUONI WA KI-HANAFI WA AL-USWUUL.
Mtindo wa Hanafi katika uandishi wa al-Uswuul ulihusisha katika kutafsiri misingi ya Uswuul kutoka kwenye maelezo ya masuala ya kisheria ambayo waliowatangulia wao kabla wamekwisha kuyajadili. Hivyo, msingi wa masomo yao ya al-Uswuul ni yale yaliyotolewa kutoka kwenye maelezo ya masuala ya kisheria yaliyokwishatatuliwa huko nyuma, na sio kwa njia nyengine ya mzunguko. Hivyo kwa mujibu wa mtindo huu, yule ambaye anasoma Uswuul al-Fiqhi, atakusanya maelezo ya masuala kuhusiana na yale ambayo Maimamu wa Kihanafi wamekwishatolea Fataawa, na baadae kuyapambanua. Kwa kupitia upambanuzi wake, ataamua msingi ambao Fataawa hizi zitatolewa.
Shah Waliyu Allaah ametoa mawazo:-
“Nimeona kwamba, baadhi yao wamedai tofauti za baina ya Abuu Haniyfah na ash-Shaafi’iy zilizopatikana kwenye Uswuul zimetaja kitabu cha al-Bazdaawiy na kwengineko. Lakini, ukweli ni kwamba; Uswuul nyingi katika hizi zilikuwa zenyewe zimetolewa kutokana na matamshi tofauti ya kisheria ya Maimamu. Mawazo yangu kwenye suala hili ni kwamba, misingi hii ya al-Uswuul kama ni amri inayosema kwamba hiyo mahsusi “al-Khaasw” ni “Mubayyan”, na wala haihitaji kufuatwa kwa tamko la “Bayaan”, kwamba maelezo yaliyoongezwa kwa andiko linalohusisha kutengua “Naskh”, kwamba maarifa ya mambo mengi “al-‘Aam” ni kukataa maneno “Qatw’iy kama ilivyo mahsusi “al-Khaasw”; ya kwamba nambari halisi za wasimulizi haziwezi kuchukuliwa kama ni hoja kwa mujibu wa hiari Tarjiyh ya wazo la mmoja au mwengine na kwamba Hadiyth za yule ambae sio Faqiyh haihitaji kujipa tabu kuitumia kwenye kesi ambapo hakuna muafaka kwa hoja; kwamba hakuna uhalali wa fikra ya kuendelea kutoka sharti ya kabla “Shart” au wasifu “Wasf” kwenda kwenye toleo la kisheria; kwamba amri “al-Amr” kwenye maandiko, daima inaonesha wajibu wa kisheria “Wujuub”; na kuendelea mbele, zote hizi ni mifano kwa misingi iliyotumika kutoa hukumu za Maimamu. Hakika, hakuna usimulizi wenye maana wa kushauri kwamba Abuu Haniyfah au wafuasi wake wawili, Muhammad na Abuu Yussuf, walijifunga na chochote miongoni mwa misingi hii ya chanzo cha utaratibu. Kama ni hivyo, basi, misingi hii haina haja tena ya kuhifadhiwa na kutetewa kama walivyofanza al-Bazdaawiy na wengineo, kuliko wanavyofanza misingi ya upinzani”.[69]
SAYANSI YA USWUUL AL-FIQHI KIPINDI CHA KARNE YA SITA HIJRIYAH NA KIPINDI KINACHOFUATA.
Kutokana na kukusanywa pamoja mada kuu za somo hili, kwa mujibu wa mtindo wa Mutakallimuun, katika kazi kuu nne: Al-Ahd, Al-Mu’tamad, al-Burhaan na al-Mustaswfa, wanazuoni wakuu wawili katika miongoni mwa Mutakallimuun walifupisha vitabu hivi vinne kwenye kazi yao wenyewe.
Wa mwanzo alikuwa ni al-Imaam al-Fakhr ad-Diyn ar-Raazi (Amefariki mwaka 606 H.), ambaye alifupisha kwenye kitabu chake cha al-Mahswuul “Kinachofikiwa na Kupatikana”, ambacho nilipata heshima ya kukichungua na kukifanyia uhariri. Kazi hii imechapishwa kwenye juzuu sita na Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Sa’ud, na hivi sasa kinachapishwa.
Wa pili alikuwa ni al-Imaam Swafiy ad-Diyn al-Amidiy (Amefariki mwaka 635 H.), ambaye alifupisha vitabu hivi vinne ndani ya kitabu chake al-Ihkaam Fiy Uswuul al-Ahkaam “Umakini kwenye Chanzo-Utaratibu wa Sheria” ambacho kimechapishwa huko Riyaadh, Cairo na kwengineko.
Vitabu hivi viwili ni vikubwa na uhakika ni rahisi kuvisoma na kuvielewa kuliko vyengine. Kati ya viwili, al-Mahswuul kimeandikwa kwa lugha nyepesi, na kina maelezo na ufafanuzi zaidi. Masahihisho na fafanuzi nyingi zimeandikwa ndani ya vitabu hivi viwili. Taaj ad-Diyn al-Armaawi (Amefariki mwaka 656) amefupisha al-Mahswuul ndani ya kitabu chake cha al-Haaswil “Toleo” ambacho kimefanyiwa uchunguzi na kuhaririwa kwa ajili ya uchunguzi wa shahada ya tatu (doctoral thesis) huko Chuo Kikuu cha Al-Azhar, lakini bado hakijachapishwa.
Al-Imaam ar-Raazi yeye mwenyewe pia amekifupisha ndani ya kitabu chenye jina la al-Muntakhab “Mateuzi” ambacho mwanazuoni mmoja anakifanyia uchunguzi na uhariri.
Al-Qaadhi al-Baydhwaawiy (Amefariki mwaka 685) amefupisha al-Haaswil ndani ya kitabu chake Minhaaj al-Wuswuul Ilaa ‘Ilm al-Uswuul “Namna ya Kuimudu Sayansi ya Chanzo-Utaratibu”; lakini ufupisho wake ulikuwa na vifupisho vingi mpaka kuwa kama fumbo, ni vigumu mno kuuelewa. Hivyo, wanazuoni wengi walichukua hatua ya kutoa fafanuzi kwenye kitabu hicho. Miongoni mwa fafanuzi hizo, kizuri chao ni kile cha al-Isnawi (Amefariki mwaka 772) ambacho kina jina la Nihaayat as-Su’l “Mwisho wa Maulizo”. Kitabu kilichokuwa macho ya wanazuoni ndani ya uwanja huu kwa muda mrefu, na bado wanazuoni wa Shafi’yah wanakitumilia.
Kitabu cha Al-Amidiy al-Ihkaam “Umakini” kilifupishwa na Ibn al-Haajib (Amefariki mwaka 645) wa fikra za kisheria za Maliki ndani ya kitabu chake cha Muntaha as-Su’l wa al-Amal Fiy ‘Ilmay al-Uswuul wa al-Jidaal “Mwisho wa Sanyansi ya Maarifa ya Sheria za Kiislamu na Hoja”, ambacho ni maarufu miongoni mwa wafuasi wa al-Imaam Maalik.
Fafanuzi bora inayoweza kupatikana kwa kazi hii ni ile ya ‘Udad ad-Diyn (Amefariki mwaka 756), ambacho masahihisho na fafanuzi kadhaa zimeandikwa.
Vitabu vyote hivi vimeandikwa kwa kufuata mtindo wa Mutakallimuun, vikitoa tafsiri ya kanuni, kuelemea ushahidi juu yake, na kutafuta kuweza kubatilisha kwa njia hizi kwa wale wenye fikra pinzani, hadi kundi moja kati ya mawili yalikubali kushindwa.
Wanazuoni wa Hanafiyyah wa Uswuul nao halkadhalika walijituma kwenye kusoma vitabu vya al-Baydhwaawiy na as-Sarkhasi. Hali hii iliendelea kama ilivyo hadi mwisho wa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba H. Pale wanazuoni wa al-Uswuul walipoanza kutumia mtindo mpya. Mtindo huu ulihusisha kuichangaya pamoja mitindo ya Mutakallimuun na wanazuoni wa Hanafiyyah ili kutoa vitabu vyenye mchanganyiko wa Uswuul kwa makundi mawili.
Kufuatia mtindo huu, Mudhwaffar ad-Diyn as-Sa’ati (Amefariki mwaka 694) aliandika Badi’i al-Nidhwaam al-Jami’i Bayna Kitabay al-Bazdaawi wa al-Ihkaam. Kitabu hichi ni kimoja miongoni mwa vinavyopatikana kwa kuchapishwa.
Sadi ash-Shari’ah (Amefariki mwaka 747) ameandika Tanq’iyh al-Uswuul “Kuisafisha al-Uswuul”, ambacho alifupisha al-Mahswuul, Uswuul al-Bazdaawi na Mukhtasar bin al-Hajiyb. Baadaye aliandika fafanuzi kwenye kitabu chake mwenyewe chenye jina la at-Tawdhwiyh “Mbayana”, ambacho at-Taftazaani (Amefariki mwaka 792) amejumlisha fafanuzi nyembamba yenye jina la at-Talwiyh. Vitabu vyote vitatu; at-Tanqiyh, at-Tawdhwiyh na at-Talwyih vinapatikana katika chapa.
Taj ad-Diyn as-Subkiy ni miongoni mwa wanazuoni wa Shafi’iiyyah ambaye ameandika kitabu chake maarufu, Jam’al al-Jawaam “Mkusanyo wa Maarifa”. Kwenye utangulizi, ametaja kwamba amekusanya kazi yake kutokana na vitabu mia moja tofauti kwenye al-Uswuul. Wanazuoni wengi wameandika fafanuzi na kuweka rejeo (footnotes) kwa kitabu cha as-Subkiy. Kati ya hizi, labda fafanuzi iliyo muhimu zaidi na yenye kupatikana kwa mapana ni Sharh al-Jalaal al-Muhalliy, ambayo inabaki hadi leo kuwa ni msingi wa masomo ya al-Uswuul, haswa kwa wanazuoni wa Shafi’iiyyah (Ki-Shafi’iy).
Badr ad-Diyn az-Zarkhaasiy (Amefariki mwaka 794) pia ameandika ufafanuzi kwa jina la Tashriyf al-Masami’iy “Kuyaridhisha Masikio”, sehemu miongoni mwa hiyo ilichapishwa nchini Cairo ikiwa na rejeo za ash-Shaykh al-Muti’i (Amefariki mwaka 1354). Mmoja miongoni mwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Imaam Muhammad bin Sa’ud amechunguza na kufanyia uhariri sehemu ya kitabu hichi hivi karibuni kwa ajili ya kutunukiwa uchunguzi kwa shahada ya tatu (doctoral thesis).
Az-Zarkhaasiy pia ameandika al-Bahr al-Muhiytw “Bahari Iliyo Kubwa Mno”, ambacho amekusanya maoni ya wanazuoni wa al-Uswuul kutoka zaidi ya vitabu mia moja. Mwanafunzi hakuacha kuchunguza na kukifanyia uhariri kitabu hicho, chini ya usimamizi wetu, kwa ajili ya kutunukiwa uchunguzi kwa shahada ya tatu (doctoral thesis), na tayari amekwishakamilisha juzuu moja na kukichapisha.
Miongoni mwa Hanaabilah, Ibn Qudaamah (Amefariki mwaka 620) ameandika Rawdhwat an-Naadhwir wa Jannat al-Manaadhir, ambacho amefupisha Mustaswfa ya al-Ghazzaaliy, na kukiongezea maelezo mengine tofauti kwenye masuala ambayo Hanaabilah hawajakubaliana na wengine. Kitabu hichi, kimechapishwa mara kadhaa, na Hanaabilah wameona manufaa ndani yake, hadi hatua ya kufikia kuvikataa takriban vitabu vyengine vyote.
Sulaymaan at-Tufi (Amefariki mwaka 716) amefupisha kazi hii, na kutoa fafanuzi kwenye ufupisho wa juzuu mbili.
Miongoni mwa Maalikiyyah, al-Qarraafiy (Amefariki mwaka 684) ameandika Tanqiyh al-Fuswuul Fiy Ikhitiswaa al-Mahswuul “Kuisafisha Sura kwa Ufupisho wa Mahswuul” Al-Qarraafiy pia ameandika fafanuzi kwenye al-Mahswuul katika juzuu kubwa yenye jina la Nafaa’is al-Uswuul “Hazina za Uswuul”, sehemu miongoni mwake imefanyiwa uchunguzi na kufanyiwa uhariri chini ya usimamizi wetu mjini Riyaadh.
[64] Angalia al-Makki, Manaaqib al-Imaam Abuu Haniyfah, II, uk. 245, Utangulizi wa Uswuul as-Sarkhasiy, 1, 3, Qutubzadeh, Miftaah, as-Sa’adah, II, uk. 37, na Ibn an-Nadiym, Al-Fihrist, Watu wote waliofanya madai haya waliegemeza maelezo yao juu ya mawazo ya Ibn an-Nadiym ndani ya maandiko ya habari za maisha ya Muhammad bin al-Hasan. “Anacho kitabu cha Uswuul chenye sura kwenye Swalaah, Zakkah na Hajj.” Hili, hata hivyo, linaonesha kuturudisha kwenye kazi ya Uswuul ad-Diyn (Ukweli ni kwamba, kinachoonesha hapa, ni kwamba kumbukumbu ni kwa kazi ya al-Imaam Muhammad bin al-Hasan kwenye Fiqh, Kitaab al-Aswl, ambacho kimechapishwa hivi punde nchini Pakistan. Na zaidi ya hapo, mawazo ya kwamba Abuu Yuusuf ameandika kwanza kuhusu Uswuul imetokana na usimuliaji uliojumuishwa na Khaatib wa Baghdad ndani ya kitabu chake cha Taariykh Baghdad).
[65] Angalia Vol. 1, u. 110-111.
[66] Kazi kuu ya al-Jassaas, Ahkaam al-Qur-aan, ilikuwa ndio mada ya Mhariri wa kazi hii ya uchunguzi, na hivi sasa kimeshatafsiriwa kwenye lugha ya Kiingereza, pamoja na kutolewa maelezo,.
[67]Taqwiym al-Adillah, kimehaririwa kwenye juzuu kumi na hivi karibuni kitachapishwa, Allaah Akipenda.
[68] Kila kundi hili la wanazuoni wameongeza kitu cha kwao kwenye vitabu vyao, ingawa walitumia mtindo mmoja wa uandishi na mtindo mmoja wa kuwasilisha ushahidi na hoja.
[69] Angalia ad-Daalawi, Hujjatullah al-Baalighah, (Misr), I, uk. 336-341; pia ad-Dahlaawi, Al-Inswaaf Fiy Bayaan Asbaab al-Ikhtilaaf, (Salafiyya, Cairo), uk. 38-40.