Vitendo Vya Sunnah Inapasa Kufanya Sajdatus-Sahw?

 

SWALI:  
 
Kutokana na swali langu la mwanzo (kuhusu vipi vitendo vya Fardhi  na vipi vitendo vya Sunnah katika Swalah)   naendelez kuuliza;
 
 je hivyo vitendo vya Sunnah ukivisahau, inakubidi ufanye "Sijdatus-sahw"?

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na Salaam zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Vitendo vya Sunnah vinapendekezeka kutekelezwa katika Swalah, kama mfano du’aa ya kufungulia Swalah, Surah ndogo baada ya Suratul-Faatihah, adkhaar katika rukuu na katika kunyanyuka na katika sujuud n.k. Lakini mtu atakaposahau vitendo hivyo halazimiki kufanya Sajdatus-Sahw.

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

Share