Anaweza Kusoma Aayatul-Kursiy Katika Kila Swalaah?
Anaweza Kusoma Aayatul-Kursiy Katika Kila Swalaah?
SWALI:
JE ninaruhusiwa kusoma ayatel al kursi kila swala??
JIBU
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hakika isiyo na shaka ni kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kusoma baadhi ya nyiradi baada ya kila Swalaah ya faradhi katika Swalaah tano kwa mchana na usiku. Miongoni na kisomo ambacho kinafaa kifanywe na Muislamu ni kusoma Ayaatul Kursiy.
Kwa hiyo, kwa muhtasari ni kuwa unafaa kusoma Ayaatul Kursiy baada ya kila Swalaah ya faradhi. Hakika ni kuwa kwa ule ubora na fadhila za Aayah hiyo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru pia tuisome wakati tumepanda kwenye vitanda vyetu kwa ajili ya kulala. Na miongoni mwa Aayah zingine, ni zile Aayah 10 katika Suratul Baqarah ambazo zinamlinda mtu na Shaytwaan.
Ama kuisoma katika kila Swalaah, haikuthibiti kuwa alifanya hivyo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Ni vizuri kufuata mafunzo kama yalivyo, hivyo ni vizuri kusoma Suwrah mbali mbali katika Swalaah.
Na Allaah Anajua zaidi