Mke Analalamika Mume Ana Mashetani Yanamfanya Asiweze Kukamilisha Tendo La Ndoa

 

SWALI:

 

Mimi ni mwana ndoa na bahati mbaya mume wangu ana matatizo ya mashetani, wakati wa tendo la ndoa huwa hawezi kufanya lolote au muda mwengine kuwa anashindwa njiani, jee Sheikh kuna dawa gani za kidini na za kiislamu ambazo mwanadamu mwenye tatizo kama hili hutumia na kuondokana na tabu hii?naomba msaada wenu ishAllaah,  Wabillah Tawfiq.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa dada yetu muuliza swali na tunapenda kukutoa wasiwasi kuwa hatuweki majina ya waulizaji.

 

Hili ni tatizo ambalo mwanaume au mwanamke anaweza kukumbwa. Akiwa mwanaume anaweza kukumbwa na jini la kike ambalo linamuhangaisha na hivyo kushindwa kumtimizia mkewe kitendo cha ndoa. Na akiwa mwanamke anaweza kukumbwa na jini la kiume ambalo linalala naye na kumuhangaisha kimapenzi hivyo kutoweza kukutana na mumewe kwani nguvu za jini ni kubwa. Baada ya jimai na mwanamke huwa mchofu hivyo kutoweza kufanya tendo la ndoa na mumewe.

 

Tatizo hilo lina tiba na tiba yake si kwenda na wachawi kama wanavyofanya wengi miongoni mwetu. Bali tiba yake mwanzo ni wewe kujitibu mwenyewe kwa kusoma kisomo cha Qur-aan na Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ambazo zinampatia kinga mwenye kusoma. Hizi inatakiwa mtu asome asubuhi na jioni. Na kinga hii huitwa Ruqyah. Unaweza zaidi kusoma kuhusu Ruqyah hapa:

 

 

Taratibu Za Ruqyah Na Yapasayo Kufanywa Kabla Ya Kusoma Ruqyah

 

 

Pia kusoma Aayah kadhaa za Suratul Baqarah (1 – 5, 255 – 257 na 284 – 286), Suratul Ikhlaas na Mu'awwidhatayn (Qul A'udhu birabbil Falaq na Qul A'udhu birabbin Naas). Na ikiwa mtu amekumbwa na jini basi anaweza kwenda kwa Shaykh mwenye kuaminika elimu yake na ucha Mungu wake ambaye atasoma baadhi ya Aayah za Qur-aan ili kumtoa, kisomo ambacho kitafahamika na kinacho kwenda sambamba na Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Soma pia Adhkaar za asbuhi na jioni kwa mfululilzo bila kuacha ni tiba na kinga kubwa:

 

Hiswnul-Muslim: Du’aa Na Adhkaar Kusoma Na Kwa Kusikiliza (Toleo Lilohaririwa)

 

027-Hiswnul-Muslim: Nyiradi Za Asubuhi Na Jioni

 

 

Soma pia Swali na jibu lifuatalo ambalo lina maelezo zaidi kuhusu matatizo kama hayo:

 

Mke Wangu Amevaliwa Na Majini Wa Mahaba? Hapendi Kutenda Kitendo Cha Ndoa Na Mimi

 

Pia ni muhimu kwa kumkinga mtoto kabla ya kuzaliwa kwa wanandoa kusoma dua wakati wanapofanya jimai nayo ni kusema duaa katika kiungo kifuatacho:

 

081-Hiswnul-Muslim: Du’aa Kabla Kujimai (Kumuingilia Mke)

 

Anasema Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akizaliwa mtoto hatasogelewa na Shaytani (al-Bukhaariy).

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share