Mwanamke Anataka Kuolewa Ndoa Ya Pili, Je, Anahitaji Idhini Ya Walii?
SWALI:
Ndugu waislam, shukurani kubwa zimwendee Allaah subhanahu wataala na mtume wetu muhammad S.A.W pamoja na wale wote walioanzisha websait hii . Suala langu
Mimi niliolewa na kuachika nikabahatika kuposwa na mchumba mwengine
ambae hatujuanikwa hiyo hakuna shaka kwenye ndoa kwa hilo, lakini kinachonikosesha raha ya maisha ni ile siku ya harusi hakuna aliyechukua
idhini kwa wazee wangu niliwaambia kama naolewa na tulikubalia na wazee wa huyu mchumba walikwenda kujuana na familia yangu.lakini siku ya harusi ilipofika niliambiwa kama madhali niliolewa na kuachwa basi haina haja kuchukuliwa idhin jee ndoa yangu mimi ipo kwenye fungu gani? Na
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri dada yetu. Ieleweke wazi kuwa ndoa yoyote ile ni lazima kuwe na walii wa mwanamke iwe ni ndoa yake ya kwanza (akiwa bikira) au ya pili (akiwa ameachwa au ni mjane). Walii kumuoza bintiye ni katika sharti la kusihi Nikaah. Hii ni kwa mujibu wa kauli ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Hapana Nikaah ila kuwepo kwa walii …” (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na Ibn Maajah kutoka kwa Abu Muusa [Radhiya Allaahu ‘anhu]).
Hivyo, mwanamke akijiozesha mwenyewe bila walii, Nikaah yake ni batili. Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Amewataka mawalii kuwaozesha wajane wao:
“Na waozeni wajane miongoni mwenu na wema katika watumwa wenu na wajakazi wenu” 924: 32).
Akasema tena (Subhaanahu wa Ta‘ala): “Basi msiwazuie kuolewa na waume zao endapo baina
Hii Aayah ya pili wanaambiwa mawalii wasiwe ni wenye kuwazuia wawili wapendao baada ya kuwa eda imemalizika kurudiana bali wanataka watoe idhini ikiwa kuna wema ndani ya kurudiana kwao.
Walii wa mwanamke ni babake, kisha aliyeusiwa naye, kisha babu mzaa baba, kisha watoto wake mwanamke, kisha watoto wao hata wakishuka chini vipi, kisha nduguze shaqiqi, kisha nduguze kwa baba, kisha watoto wao, kisha ‘ami shaqiqi, kisha ‘ami kwa baba tu, kisha watoto wao. Kisha jamaa zake wa karibu na kisha hakimu ikiwa hana jamaa kabisa.
Tunakutakia kila la kheri na fanaka katika ndoa yako.
Na Allaah Anajua zaidi