Mume Anayedai Kujua Dini Anaishi Naye Bila Nikaah Akidai Kuwa Inatosheleza Baba Wa Mke Kupokea Mahari Na Sasa Mja Mzito
SWALI:
Asalam alaikum
Mimi naomba kuuliza swali ambalo nadhani ni la ajabu lakini natumai mutanipa ufaafanuzi nielewe. mimi nimeolewa lakini kabla ya kuolewa posa yangu ilikua ni ya utata sana hadi ikapita kama mwaka mmoja mzima kwa subra, mume wangu alhamdullilahi ni mtu aliye shika dini na mwenye elimu ndio sababu ya kukubali kuolewa na yeye ili nami nipate faida kwake lakini mushkil wangu ni kuwa hatukufanya nikah akidai kua si lazima kufanya nikah madhali baba amekubali, mahari imekubalika na mimi mwenyewe nimekubali.....kulingana na ilmu yake anasema kua ana ushahidi kua nikah si lazima kwa wanandoa. Kabla sijakutana naye nilimwambia kua ni lazima tufanye nikah hata
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kufunga Nikaah na mume unayempenda.
Hakika ni ajabu kwa mtu unayesema ana elimu ya dini lakini akashindwa kufahamu muongozo wa Uislamu kuhusu ndoa. Uislamu ni nidhamu katika kila jambo lake, kubwa au dogo. Na ndoa haiko nje ya nidhamu hiyo na hivyo ikawekewa masharti ili wanaume na wanawake wasiwe ni wenye kuchukuana tu au kuketi bila ndoa ya halali. Na jambo
Masharti ya kusihi ndoa ya Kiislamu ni
1. Kukubali kwa mume kuoa na mke kuolewa. Bila idhini hiyo hakuna ndoa baina ya mume na mke.
2. Idhini ya walii – baba au jamaa ya karibu ya mke aliyepatiwa jukumu la kutoa idhini. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Hapana ndoa bila ya walii” (Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na al-Haakim).
3. Ni lazima kuwe na mashahidi wawili waadilifu wakiwa zaidi ya hao ni bora zaidi. Na amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hapana ndoa isipokuwa kwa walii na mashahidi wawili waadilifu” (ad-Daraqutwniy na al-Bayhaqiy).
4. Kuwe na Khutbah, ambayo inatakiwa ifungwe na baba mzazi wa msichana. Na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia
5. Mume kulipa mahari aliyotaka msichana. Na mahari ni wajibu kwa kauli ya Aliyetukuka: “Na wapeni wanawake mahari
Masharti hayo yaliyo juu yakikamilika basi ndoa hiyo inakuwa ni ya Kiislamu na mume na mke ni wa halali kukaa pamoja. Ikiwa baadhi yake hayakufanyika basi inakuwa wewe na mumeo mumekaa pamoja nje ya shari’ah ya Kiislamu, hivyo kuchukuliwa kuwa mnazini tu.
Inafaa ujiepushe na utata huo ambao tayari umeingia ndani yake. Na ni ajabu kuwa baba yako amekubali wewe ukae na aliyekuposa katika hali
Rejea haraka katika haki na jiepushe na hayo maisha mnayoishi hivi sasa yasiyo ya Kiislam. Na fahamu kuwa huyo mwanaume hajui dini na ni katika wajanja tu wanaotaka kupata mahitajia
Na Allaah Anajua zaidi