Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Vipi Kumswalia
Fadhila Za Kumswalia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Na Vipi Kumswalia
Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni amri ya Allaah (سبحانه وتعالى) kama Anavyosema:
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa mamkizi ya amani na kwa tasliymaa. [Al-Ahzaab (33: 56)]
Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:
إِنَّ اللَّـهَ وَمَلَائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ ۚ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٥٦﴾
Hakika Allaah na Malaika Wake wanamswalia Nabiy. Enyi walioamini mswalieni na msalimieni kwa maamkizi ya amani na kwa tasliymaa. [Al-Ahzaab 33: 56]
Maana ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): Ni kumsifia kwa Malaika, kumteremshia rahmah na baraka, fadhila n.k.
Maana ya Malaika Wake kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) du’aa Amghufurie na Amteremshie baraka.
Maana ya Waumini kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ni kumuombea kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) du’aa na amani. Juu ya hivyo Waumini kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) inawarudia wenyewe thawabu tele kutokana na fadhila zilizotajwa katika Hadiyth kadhaa za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), miongoni mwazo ni:
Fadhila Za Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
1-Kupata thawabu mara kumi kwa kumswalia mara moja:
عنْ عبد اللَّه بن عمرو بن العاص رضي اللَّه عنْهُمَا أنَّهُ سمِع رسُول اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ: ((مَنْ صَلَّى عَلَيَّ صَلاَةً، صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ بِهَا عشْراً)) رواهُ مسلم
Imetoka kwa 'Abdullaah bin 'Amru bin Al'-Aasw (رضي الله عنهما) kwamba kamsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: ((Atakayeniswalia mara moja, Allaah Atamswalia mara kumi)) [Muslim]
2-Kupata ukaribu wa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Peponi:
عن ابن مسْعُودٍ رضي اللَّه عنْهُ أنَّ رسُول اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال : (( أَوْلى النَّاسِ بي يوْمَ الْقِيامةِ أَكْثَرُهُم عَليَّ صلاةً)) رواه الترمذي وقال : حديثٌ حسنٌ
Imetoka kwa ibn Mas'uwd (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Watu wa mwanzo kwangu (watakaokuwa karibu yangu) siku ya Qiyaamah ni wale wanaoniswalia sana)). [At-Tirmidhy na kasema ni Hadiythi Hasan]
3-Roho ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hurudishwa mwilini mwake apokee na arudishe Salaam:
عنْ أبي هُريْرةَ رضي اللَّه عنهُ أنَّ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم قال: ((ما مِنْ أحد يُسلِّمُ علَيَّ إلاَّ ردَّ اللَّه علَيَّ رُوحي حَتَّى أرُدَّ عَليهِ السَّلامَ)) رواهُ أبو داود بإسناد صحيحٍ
Imetoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Yeyote atakayeniswalia hurudishiwa roho yangu hadi nimrudishie salaam)) [Abuu Daawuwd kwa Isnaad ya Hasan]
4-Popote ulipo Unapmswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kunamfikia:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لاَ تَجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قُبُورًا، وَلاَ تَجْعَلُوا قَبْرِي عِيدًا، وَصَلُّوا عَلَيَّ فَإِنَّ صَلاتَكُمْ تَبْلُغُنِي حَيْثُ كُنْتُمْ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ بِإِسْنَادٍ حَسَنٍ وَرُوَاتُهُ ثِقَاتٌ
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Msifanye nyumba zenu makaburi, wala msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kurejewa rejewa na niswalieni, kwani kuniswalia kwenu kunanifikia popote mlipo)) [Abuu Daawuwd kwa isnaad Hasan ya wasimuliaji wanaotegemewa]
Makemeo Ya Kutokumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
1-Asiyemswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapotajwa amepewa sifa ya ubakhili:
وعن علِيٍّ رضي اللَّه عنْهُ قال: قال رسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((الْبخِيلُ من ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَم يُصَلِّ علَيَّ)) رواهُ الترمذي وقالَ : حديثٌ حسنٌ صحيحٌ .
Imetoka kwa 'Aliy (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Bakhili ni yule ambaye nimetajwa kwake na hakuniswalia)) [At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan Swahiyh]
2-Asiyemswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anapotajwa hupata khasara:
عنْ أبي هُريْرةَ رضي اللَّه عنهُ قال: قال رسُولُ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((رَغِم أنْفُ رجُلٍ ذُكِرْتُ عِنْدَهُ فَلَمْ يُصَلِّ علَيَّ)) رواهُ الترمذي وقالَ : حديثٌ حسنٌ .
Imetoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Amepata khasara mtu ambaye nimetajwa kwake na hakuniswalia)) [At-Tirmidhiy na kasema Hadiyth Hasan]
Mapendekezo Ya kumswalia Siku ya Ijumaa:
عَنْ أَوْسِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ مِنْ أَفْضَلِ أَيَّامِكُمْ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَأَكْثِرُوا عَلَيَّ مِنْ الصَّلاةِ فِيهِ، فَإِنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ)) قَالوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تُعْرَضُ صَلاتُنَا عَلَيْكَ وَقَدْ أَرَمْتَ؟ قَالَ: يَقُولُ: بَلِيتَ قَالَ: ((إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَرَّمَ عَلَى الأَرْضِ أَجْسَادَ الأَنْبِيَاءِ)) رواه ابو داوُود بِاِسنادٍ صحيح
Imepokelewa kutoka kwa Aws bin Aws (رضي الله عنه) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم ) amesema: ((Hakika siku zenu zilizo bora mno ni siku ya Ijumaa, basi kithirisheni kuniswalia siku hiyo, hakika Swalaah zenu huwa naletewa)). Maswahaba wakauliza: “Ee Rasuli wa Allaah! Vipi Swalaah zetu kuwa unaletewa na ilihali wakati huo utakuwa umeshaoza?” Akajibu: ((Hakika Allaah Ameiharamisha ardhi kula viwiliwili vya Manabii)). [Abuu Daawuwd kwa Isnaad Swahiyh]
Pia:
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، أَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: (( خَيْرُ يَوْمٍ طَلَعَتْ عَلَيْهِ الشَّمْسُ يَوْمُ الْجُمُعَةِ فِيهِ خُلِقَ آدَمُ وَفِيهِ أُدْخِلَ الْجَنَّةَ وَفِيهِ أُخْرِجَ مِنْهَا وَلاَ تَقُومُ السَّاعَةُ إِلاَّ فِي يَوْمِ الْجُمُعَةِ))
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Siku bora kabisa iliyochomoza jua ni siku ya Ijumaa, na hiyo ndio ameumbwa Aadam na hiyo ndio aliingizwa Jannah (Peponi) na akatolewa humo. Na Qiyaamah hakitosimamia siku yoyote isipokuwa siku ya Ijumaa)) [Muslim]
Vipi Kumswalia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
Alipoulizwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) jinsi gani kumswalia alijibu kuwa ni kumswalia kama vile tunavyomswalia ndani ya Swalaah katika kikao cha Tashahhud pale kwenye du’aa inayoitwa Swalaatu Ibraahimiyyah (Swalaah ya Ibrahiym) ambayo imekuja katika matamshi mbali mbali yanayotofautiana kidogo; mojawapo ni kama ifuatavyo:
Allaahumma Swalli ‘alaa Muhammadin, wa ‘alaa aali Muhammadin, kamaa Swallayta ‘alaa Ibraahiyma, wa ‘alaa aali Ibraahiyma, Innaka Hamiydun Majiydun, Allaahumma Baarik ‘alaa Muhammadin wa ‘alaa aali Muhammadin kamaa Baarakta ‘alaa Ibraahiyma wa ‘alaa aali Ibraahiyma Innaka Hamiydun Majiydun
Ee Allaah! Mswalie Muhammad, na ahli wa Muhammad kama Ulivyomswalia Ibraahiym na juu ya ahli zake Ibraahiym, hakika Wewe ni Mwenye kustahiki kuhimidiwa, Mwenye utukufu. Eee Allaah! Mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama Ulivyombariki Ibraahiym na juu ya ahli zake Ibraahiym, hakika Wewe Ni Mwenye kustahiki kuhimidiwa, Mtukufu.