Mwanamke Aliyekwishaolewa Kabla - Anahitaji Walii? Na Ndoa Ya Pili Inaruhusiwa Kuwa Ya Siri
SWALI:
Mwanamke kaolewa na kashaachwa kakaa miaka 10 sasa anataka kuolewa na anataka kuolewa siri jee inatosha yeye mwenyewe kutoa idhini na kuwaita mashahidi pamoja na shekhe kwa ajili ya ndoa nb mwanamke huyo babayake yuko hai lakini huyu mume kampa masharti kuwa ni lazima iwe siri jee ndoa itafaa au haifai
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Hakika ni kuwa kila jambo katika Uislamu lina masharti kusihi kwake. Lau masharti
Miongoni mwa mojawapo ya masharti ya ndoa ni kupatikana kwa walii wa mwanamke, akiwa ni bikira au thayyib (aliyeolewa hapo mbeleni). Na haingii akilini haswa kwa Muislamu iwe ndoa itafanywa waalikwe mashahidi wawili na pia wamualike Shaykh wa kuozesha lakini baba asialikwe. Baba ni mtu muhimu na ndiye anayetakiwa atoe ridhaa katika jambo
Na katika sharti ya ndoa ni lazima kuweko walii
((Hakuna Nikaah ila kwa Walii)) [Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah na ameisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Sahihi ya At-Tirmidhiy]
Vile vile Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((Mwanamke yeyote akiolewa bila ya Walii wake basi Nikaah yake ni baatil, Nikaah yake ni baatil, Nikaah yake ni baatil)) [Ahmad, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy na kaisahihisha Shaykh Al-Albaaniy katika Swahiyhul-Jaami'i]
Kufanywa ndoa katika hali hiyo ni kuwa mwanamke anaficha kitu muhimu. Tuelewe ndoa
Hivyo, nasaha kwetu kwa ndoa anayetaka kuolewa ni amfahamishe baba mzazi kabla ya shughuli hiyo.
Na Allaah Anajua zaidi