Mwanamume Aliye Na Uwezo Wa Kuoa Na Hakuoa Hadi Amefariki Nini Hukmu Yake?

 

SWALI:

Sheikh ni nini hukum ya kijana wa kiisilamu ambaye ameacha kuo ili hali anasifa zote za kuoa halafu akapatwa na mauti bila kuoa

 


 

JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Hakika wanachuooni wameigawa ndoa kwa sampuli zifuatazo:

 

  1. Ndoa iliyo Wajibu: Ikiwa Muislamu hawezi kujizuilia na zinaa naye ana uwezo basi kwake inakuwa ni lazima aoe.

  2. Ndoa iliyo Haramu: Ikiwa Muislamu hana uwezo wa kutekeleza tendo la ndoa basi kwake inakuwa ni haramu kuoa.

  3. Ndoa ya Sunnah: Ikiwa Muislamu ana uwezo wa kujizuilia na kutooa kwake hakumpeleki kabisa katika zinaa, basi kwake si lazima. Mbali na kuwa kuoa kuna fadhila kubwa sana katika Dini yetu.

Hakika ni kuwa wapo wanachuoni wakubwa kama Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah na Imaam Abu Zakariyya Yahyaa bin Sharaf bin Hasan an-Nawawiy ambao hawakuoa kwa sababu moja au nyengine.

Kwa hiyo, kijana huyo hana makosa yoyote bali ingekuwa bora kwake kama angeoa.

Inaonekana unamjua vilivyo huyo kijana lakini wakati mwingine unaweza kumuona kijana kama huyo ukaona ana sifa zote lakini ukweli ukawa ana upungufu ambao wewe huujui wala yeye hautaji.

Inafaa tuwahimize vijana pamoja na kuwasaidia ili watekeleze Sunnah hii muhimu sana katika maisha ya hapa duniani.

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share