Wazazi Hawataki Niolewe Ndoa Ya Pili Na Mume Aliye Mdogo Kwangu
SWALI:
Asalam alaykum jamii yote ya kiislam pamoja na ndugu zengu wote mlioko hapa al hidaya mimi ninasuala langu muhimu ambalo linanisumbuwa akili yangu na sitaki kujamulia mwenyewe mpaka nipate jawabu kutoka kwa wislamu wenzangu.
mimi ni mwanamke ambaye niliolewa kama miaka 10 nyuma lakini baada yahapo ilitokea misukosuko mengi naikawa ndowa yangu ilisha na tukaamuwa kuachana na mume wangu natokea nimeachwa sasa ni miezi 8 natalaka zimeisha tayari.na nimezaa watoto watatu na sasa imetokea kheri nyengine lakini uzito uko kwa wazazi wangu kuwa haitaki hii ndowa iwe kutokana na huyu kijana ni mdogo kwa umri .nikuwa kama atanipotezea time yangu kwakweli tumepishana kwa age yeye ni 25 na mimi 30 na huyo kijana nimeulizia kwa watu na nimeambiwa nikijana mzuri hata kwa tabia. nategemea kupata jibu zuri kutoka kwenu, ahsanteni
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako. Jamii yetu ya Waislamu hasa Afrika Mashariki ina matatizo mengi ambayo inairudisha nyuma hasa katika mas-ala ya kijamii. Na katika matatizo ambayo yameikumba kwa kiasi kikubwa zaidi mpaka ikakaribia kuisambaratisha jamii hii ni katika mas-ala ya ndoa. Jamii yetu iko nyuma
Pia kwa kiasi kikubwa hatuna malezi muruwa katika suala hili. Hivyo, linapokuja tatizo wazazi hutaka kujiamulia hatima ya binti
Ingekuwa wazazi wanaielewa Dini basi wangechukua uamuzi muafaka kabisa na kuondosha utata aina yoyote. Uislamu haujakataza mwanamme kumuoa mwanamke aliye mkubwa kumliko yeye. Tunafahamu kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuoa Khadiyjah bint Khuwaylid (Radhiya Allaahu 'anha) aliyekuwa mkubwa wake kwa miaka 15. Tunaposoma katika Siyrah tunaona jinsi gani ndoa hiyo ilivyokuwa na ufanisi wa hali ya juu mpaka mafungamano
Umri wa wanandoa si muhimu kukiwa na masikilizano. Itabidi uzungumze na wazazi wako na uwaeleze kwa njia nzuri kuhusu hayo. Ikiwa umepata habari kwa kuelezwa na unaowaamini kuwa huyo ni kijana nzuri basi itakuwa kheri. Japokuwa tungekunasihi pia uswali Swalah ya Istikhaarah kumtaka ushauri Allaah Aliyetukuka katika mas-ala hayo.
Na ikiwa wazazi bado hawataki kukuozesha kwa sababu zao nyingine ambazo hazikubaliki kisheria basi una haki kutafuta njia nyingine uweze kuolewa na huyo kijana. Kwanza utafute jamaa zako wa karibu kama ami au mjomba au kaka ili wawe
Maelezo zaidi soma maswali katika viungo vifuatavyo:
Wazazi Hawataki Nifunge Ndoa Hadi Nimalize Kusoma Nami Niko Katika Zinaa, Nifanyeje?
Na Allaah Anajua zaidi