Mke Anamlazimisha Mume Kuhusu Matumizi Ya Pesa

 

SWALI:

wassallam ndugu zangu waislamu nyote, nimekwama nilikuwa na suala langu naomba msaada wa jibu, suala langu liko kama hivi: (katika ndoa mke anatakiwa kumlazimisha mume kuhusu mambo ya pesa)

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika  Salaam hazifai kufupishwa kwa kuandikwa (A.A) au (A.A.W.W.) au kama ulivyoandika kwani haijafundishwa hivyo na pia ni kujikosesha fadhila za Salaam kama tulivyoelezwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hivyo nayo tujizoeshe kuandika (Assalaamu ‘alaykum) au (Assalaamu ‘alaykum wa rahmatullaah) au (Assalaamu ‘alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh) kwa ukamilifu na tutakuwa tumeiga mafunzo ya Mtume wetu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na pia tutakuwa tumezoa thawabu zote za Salaam kama tulivyofundishwa. Na Mafunzo yote na fadhila zake zimo Alhidaaya katika kiungo kifuatacho: Maamkizi Ya Kiislamu.  

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu masrufu ya nyumba. Ni jambo linaloeleweka kwa Waislamu wote kuwa matumizi ya nyumbani yote kama ijara ya nyumba, chakula, matibabu, mavazi na kadhalika ni juu ya mume.

Mume kutofanya hivyo atakuwa amekiuka maagizo ya Uislamu na hivyo atakuwa anapata dhambi na mke anaweza kumshitaki kwa hilo. Mke analofaa kufanya ni kumkumbusha mumewe awe ni mwenye kutekeleza wajibu wake kulingana na uwezo wa mume. Haifai kwa mke kumlazimisha mumewe kwa matumizi asiyoweza. Kwa ajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Anasema:

Na juu ya baba yake chakula cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada. Wala halazimishwi mtu ila kwa kadiri ya uwezo wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mwanawe, wala baba kwa ajili ya mwanawe” (2: 233).

Aayah hiyo ipo wazi katika wajibu huo wa mume.

Na Allaah Anajua zaidi

Share