Mchuzi Wa Nyama Ya Kusaga Na Mayai
Mchuzi Wa Nyama Ya Kusaga Na Mayai
Vipimo
Nyama ya kusaga - 2 LB (Ratili)
Mayai - 6
Vitunguu - 4
Kitunguu saumu(thomu/galic) na Tangawizi - 1 Kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Nyanya iliyokatwa katwa - 4
Kotmiri - ½ Kikombe
Pilipili Manga - ¼Kijiko cha chai
Bizari ya curry - ½ Kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 3 Vijiko vya supu
Garam masala - 1 Kijiko cha supu
Mafuta ya kukaangia - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha mayai, yakiiva ambua maganda na uweke kando.
- Katika sufuria weka mafuta yapate moto, Kaanga vitunguu hadi vigeuke na kuwa rangi ya hudhurungi.
- Halafu tia thomu na tangawizi kanga kidogo tu, kisha tia bizari zote na pilipili uendelee kukaanga.
- Kisha weka nyama na uiache motoni huku unakoroga hadi iwe si nyekundu tena.
- Tia nyanya na chumvi ziache zilainike halafu tia nyanya ya kopo.
- Ongeza maji kiasi unavyopenda mchuzi wako kuwa mzito au mwepesi.
- Kisha weka yale mayai ya kuchemsha na iache itokote kidogo kwa moto mdogo.
- Mwishoe mwagia kotmiri, changanya na umimine katika bakuli na itakuwa tayari kwa kuliwa na wali au mkate upendayo.