Mchuzi Wa Kamba (Prawns) Kwa Sosi Ya Nyanya Na Kotmiri
Mchuzi Wa Kamba (Prawns) Kwa Sosi Ya Nyanya Na Kotimiri
Vipimo
Kamba - 1 Lb
Vitunguu - 3 katakata
Nyanya - 4 zisage
Pilipili za kijani - kiasi 3
Kitunguu saumu (thomu/garlic) - 1 kijiko cha chai
Tangawizi - 1 kijiko cha chai
Uzile (bizari ya pilau ya unga-Jiyra) - ½ kijiko cha chai
Bizari ya mchuzi - 1 kijiko cha chai
Pilipili ya unga - ½ kijiko cha chai
Nyanya ya kopo - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Ndimu - nusu kamua
Kotimiri - kiasi katakata
Mafuta - 1/4 kikombe
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya kamba na thomu, tangawizi, pilipili manga, pilipili ya unga, jira, na chumvi.
- Katakata vitunguu weka pembeni.
- Katakata pilipili sehemu mbili kwa urefu.
- Saga nyanya au katakata weka pembeni.
- Weka mafuta katika kikaangio au sufuria.
- Kaanga vitunguu hadi vigeuke rangi ya ligh brown.
- Tia nyanya na tia nyanya kopo kaanga kidogo
- Tia bizari ya mchuzi
- Tia maji kidogo upate sosi.
- Tia kamba uache katika moto, koroga uache kamba wapikike (kama ni wa freezer hawachukui muda kuiva).
- Tia ndimu kidogo
- Mwagia kotimiri ulokatakata, ikiwa tayari kuliwa
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)