Kuku Kidari Kwa Sosi Ya Malai
Kuku Kidari Kwa Sosi Ya Malai
Mahitajio |
Utayarishaji |
Kipimo
|
Kuku bila ya mfupa (kidari) |
katakata osha |
1 kilo |
Kitunguu maji |
katakata (chop) |
2 |
Tungule/nyanya |
“ |
2 |
pilipili mbichi/shamba kijani |
Saga |
3 |
Kitunguu thomu/saumu |
katakata (chop) |
7-10 chembe |
Tangawizi mbichi |
saga |
1 kipande |
chumvi |
|
kiasi |
Pilipili nyekundu ya unga |
|
1 kijiko cha chai |
Malai (cream) |
tumia ya tayari |
1 gilasi |
Bizari pilau/ jiyrah/cummin |
|
1 kijiko cha chai |
Gilgilani/Dania/corriander |
|
1 kijiko cha chai |
Mafuta |
|
1/3 kikombe |
Namna Ya Kupika:
- Weka mafuta katika sufuria, kaanga vitunguu maji hadi vilainike- Usiache mpaka vikageuka rangi sana.
- Tia kitunguu thomu/saumu na tangawizi mbichi endelea kukaanga.
- Tia vipande vya kuku, endelea kukaanga kidogo
- Tia nyanya, bizari zote, chumvi, pilipili mbichi endelea kukaanga
- Mwishowe tia malai , changanya vizuri, acha ichemke kidogo kuku aive.
- Ongezea malai mwishoni baada ya kuzima moto, changanya vizuri, epua.