Matunda Mchanganyiko Na Malai
Matunda Mchanganyiko Na Malai
Vipimo
Embe- 3
Zabibu - 2 vikombe
Stroberri - 1 kikombe
Shammaam (tikiti cantelope) - ½
Tikiti la asali (honey dew) - ½
Tofaha (apples) - 2
Peaches - 3
Papayi - ½
Juisi ya embe - 2 vikombe
Malai (Cream) - 1 kikombe
Namna Ya Kutayarisha
- Menya na katakata matunda yote isipokuwa zabibu utie katika bakuli
- Mimina juisi ya embe uchanganye vizuri
- Mwagia malai (cream) katikati au tia unapopakua katika vibakli vyake.
- Unaweza kulia pia na iskrimu (ice-cream) upendayo.
Kidokezo:
Unaweza kubadlisha matunda, kuongeza au kupungza upendavyo.
