22-Hadiyth Al-Qudsiy: Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa, Kumlisha Aliye Na Njaa Na Kunywesha Aliye Na Kiu
Hadiyth Al-Qudisy
Hadiyth Ya 22
Fadhila Za Kutembelea Mgonjwa, Kumlisha Aliye Na Njaa Na Kunywesha Aliye Na Kiu
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يَقُولُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ: يَا ابْنَ آدَمَ مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدْنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَعُودُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّ عَبْدِي فُلَانًا مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَنِي عِنْدَهُ؟ يَا ابْنَ آدَمَ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمْنِي ، قَالَ: يَا رَبِّ وَكَيْفَ أُطْعِمُكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ: أَمَا عَلِمْتَ أَنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ؟ أَمَا عَلِمْتَ أَنَّكَ لَوْ أَطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟ يَا ابْنَ آدَمَ اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي، قَالَ: يَا رَبِّ كَيْفَ أَسْقِيكَ وَأَنْتَ رَبُّ الْعَالَمِينَ؟ قَالَ اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلَانٌ فَلَمْ تَسْقِهِ، أَمَا إِنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ وَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي؟)) مسلم
Kutoka Kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: ((Hakika Allaah ‘Aliyetukuka na Jalali Atasema siku ya Qiyaamah: Ee mwana wa Adam, Niliumwa na usije kunitembelea? Atasema: Ee Rabb (Mola), vipi nije kukutembelea nawe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani ulijua kuwa mja wangu fulani alikuwa mgonjwa na hukwenda kumtembelea! Hukujua kuwa ungekwenda ungalinikuta Niko pamoja naye? Ee mwana wa Adam, Nilikuomba chakula na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa chakula na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Kwani hukujua kuwa mja wangu fulani alikuomba chakula na hukumpa? Hukujua kuwa ungalimpa chakula ungalikuta hayo (jazaa) kwangu mimi? Ee mwana wa Aadam, nilikuomba maji na hukunipa. Atasema: Ee Rabb, vipi nitakupa maji na Wewe ni Rabb wa ulimwengu? Atasema: Mja wangu fulani alikuomba maji na hukumpa. Hukujua kwamba ungalimpa maji ungalikuta hayo (jazaa) Kwangu Mimi)) [Muslim]