23-Hadiyth Al-Qudsiy: Kiburi Ni Joho Langu Na Utukufu Ni Kanzu Yangu Atakayeshindana Nami Nitamvurumisha Motoni
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 23
Kiburi Ni Joho Langu Na Utukufu Ni Kanzu Yangu,
Atakayeshindana Nami Nitamvurumisha Motoni
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ هَنَّادٌ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((قَالَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ الْكِبْرِيَاءُ رِدَائِي وَالْعَظَمَةُ إِزَارِي فَمَنْ نَازَعَنِي وَاحِدًا مِنْهُمَا قَذَفْتُهُ فِي النَّارِ)) أبو داود ، ابن ماجه و أحمد
Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) ambaye amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Amesema: Kiburi ni joho Langu, na utukufu ni kanzu Yangu, yule ashindanaye na Mimi katika kimoja katika hayo nitamvurumisha Motoni)) [Abu Daawuwd, Ibn Maajah na Ahmad]