40-Hadiyth Al-Qudsiy: Mambo Yaliyozungushiwa Jannah Na Moto

Hadiyth Al-Qudsiy

Hadiyth Ya 40  

Mambo Yaliyozungushiwa Jannah Na Moto

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ عَنْ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لَمَّا خَلَقَ اللَّهُ الْجَنَّةَ وَالنَّارَ أَرْسَلَ جِبْرِيلَ إِلَى الْجَنَّةِ فَقَال: انْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ:  فَجَاءَهَا وَنَظَرَ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعَدَّ اللَّهُ لِأَهْلِهَا فِيهَا.  قَالَ:  فَرَجَعَ إِلَيْهِ قَالَ: فَوَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ، فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَانْظُرْ إِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  قَالَ: فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَإِذَا هِيَ قَدْ حُفَّتْ بِالْمَكَارِهِ،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خِفْتُ أَنْ لَا يَدْخُلَهَا أَحَدٌ. قَالَ: اذْهَبْ إِلَى النَّارِ فَانْظُرْ إِلَيْهَا وَإِلَى مَا أَعْدَدْتُ لِأَهْلِهَا فِيهَا،  فَإِذَا هِيَ يَرْكَبُ بَعْضُهَا بَعْضًا،  فَرَجَعَ إِلَيْهِ فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَا يَسْمَعُ بِهَا أَحَدٌ فَيَدْخُلَهَا، فَأَمَرَ بِهَا فَحُفَّتْ بِالشَّهَوَاتِ فَقَالَ: ارْجِعْ إِلَيْهَا فَرَجَعَ إِلَيْهَا فَقَالَ: وَعِزَّتِكَ لَقَدْ خَشِيتُ أَنْ لَا يَنْجُوَ مِنْهَا أَحَدٌ إِلَّا دَخَلَهَا)) الترمذي و قال حديث حسن صحيح – ابو داود والنسائي

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Allaah Alipoumba Jannah na moto, Alimtuma Jibriyl Jannah Akimwambia: Iangalie na angalia matayarisho Niliyoyaandaa  kwa ajili ya wakaazi wake. Akasema: Kwa hivyo alikuja kuiangalia na kuangalia maandalizi Aliyoyaandaa Allaah kwa ajili ya wakaazi Wake. Akasema: Akarejea kwa Allaah na kusema: Naapa kwa Utukufu Wako, hakuna atakayesikia (habari yake) ila tu ataingia (Jannah). Kisha Akaamrisha izungushwe mambo magumu watu wasiyoyapenda, Akasema: Rejea na angalia yale Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakaazi wake. Akasema: Kisha akarejea na akakuta imezungukwa na mambo magumu watu wasiyoyapenda. Hapo alirejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako, nina khofu hakuna hata mtu mmoja atakayeingia. Akasema: Nenda motoni ukauangalie na uangalie Niliyoyaandaa kwa ajili ya wakaazi wake. Akaona ulikuwa na matabaka moja juu ya tabaka jengine. Akarejea kwa Allaah na akasema: Naapa kwa Utukufu Wako hakuna hata mmoja ausikiae (sifa zake) atakayeingia. Kisha Allaah Aliamrisha Uhusishwe na shahawa, matamanio ya nafsi). Kisha Allaah Akamuambia: Rejea tena (motoni). Alirejea tena na akasema: Naapa kwa Utukufu, wako nakhofia kuwa hapatakuwa na yeyote atakayenusurika nao)) [At-Tirmidhiy akasema ni Hadiyth Hasan, na Abu Daawuwd na An-Nasaaiy]

 

Share