41-Hadiyth Al-Qudsiy: Jannah Na Moto Vilishindana Allaah Akahukumu Baina Yake
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 41
Jannah Na Moto Vilishindana Allaah Akahukumu Baina Yake
عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((احْتَجَّتْ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَقَالَتْ النَّارُ: فِيَّ الْجَبَّارُونَ وَالْمُتَكَبِّرُونَ، وَقَالَتْ الْجَنَّةُ: فِيَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَمَسَاكِينُهُمْ، قَالَ: فَقَضَى بَيْنَهُمَا: إِنَّكِ الْجَنَّةُ رَحْمَتِي أَرْحَمُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ، وَإِنَّكِ النَّارُ عَذَابِي أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ، وَلِكِلَاكُمَا عَلَيَّ مِلْؤُهَا)) البخاري، مسلم و الترمذي
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jannah na moto vilishindana. Moto ulisema: Ndani yangu wamo wenye kujifanya majabari na wenye kutakabari. Jannah ikasema: Ndani yangu wamo watu dhaifu na maskini. Akasema: Allaah Akahukumu baina yao: (Akasema): Wewe Jannah ni rahmah Zangu, kupitia kwako wewe Humrehemu Nimtakaye. Nawe moto ni adhabu Yangu, kupitia kwako wewe ninawaadhibu wale niwatakao na kila mmoja katika nyinyi mtajaa)) [Al-Bukhaariy, Muslim na At-Tirmidhiy]