43-Hadiyth Al-Qudsiy: Nani Aapaye Kwamba Allaah Hatomghufuria Fulani?
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 43
Nani Aapaye Kwamba Allaah Hatomghufuria Fulani?
عَنْ جُنْدَبٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حَدَّثَ ((أَنَّ رَجُلًا قَالَ: وَاللَّهِ لَا يَغْفِرُ اللَّهُ لِفُلَانٍ ، وَإِنَّ اللَّهَ تَعَالَى قَالَ: مَنْ ذَا الَّذِي يَتَأَلَّى عَلَيَّ أَنْ لَا أَغْفِرَ لِفُلَانٍ ، فَإِنِّي قَدْ غَفَرْتُ لِفُلَانٍ وَأَحْبَطْتُ عَمَلَكَ)) أَوْ كَمَا قَالَ – مسلم
Imepokelewa kutoka kwa Jundabi (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amehadithia: ((Mtu mmoja alisema: Wa-Allaahi, Allaah Hatomghufuria fulani kwa haya, Allaah Ta’aalaa Akasema: Ni nani huyo aapaye kwa Jina Langu kuwa Sitamghufuria fulani? Basi kwa yakini Nimemghufuria (huyo) fulani na Nimeporomosha 'amali zako.)) (au kama alivyosema). [Muslim]