44-Hadiyth Al-Qudsiy: Sifa Za Anayependeza Zaidi Kwa Allaah
Hadiyth Al-Qudsiy
Hadiyth Ya 44
Sifa Za Anayependeza Zaidi Kwa Allaah
عَنْ أَبِي أُمَامَةَ عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((إِنَّ أَغْبَطَ أَوْلِيَائِي عِنْدِي لَمُؤْمِنٌ خَفِيفُ الْحَاذِ ذُو حَظٍّ مِنْ الصَّلَاةِ أَحْسَنَ عِبَادَةَ رَبِّهِ وَأَطَاعَهُ فِي السِّرِّ وَكَانَ غَامِضًا فِي النَّاسِ لَا يُشَارُ إِلَيْهِ بِالْأَصَابِعِ وَكَانَ رِزْقُهُ كَفَافًا فَصَبَرَ عَلَى ذَلِكَ)) ثُمَّ نَقَرَ بِيَدِهِ فَقَالَ: ((عُجِّلَتْ مَنِيَّتُهُ قَلَّتْ بَوَاكِيهِ قَلَّ تُرَاثُهُ)) الترمذي (وكذلك أحمد وابن ماجه ) وإسناده حسن
Abuu Umaamah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amehadithia kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwamba Allaah Amesema: “Hakika anayependeza zaidi Kwangu ni Muumini mwenye hali duni, mswalihina mwenye kumwabudu vizuri kabisa na kumcha kwa siri, ambaye si maarufu kwa watu na wala hatambuliki na ambaye rizki yake ni ndogo kiasi cha kumtosheleza tu, lakini anastahamili hali hiyo.” Kisha Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akatikisa mkono wake akasema: “Kama mauti yangemfikia mapema asingekuwa na watu wengi wa kumlilia, na urithi wake ungelikuwa mdogo sana.” [At-Tirmidhiy, Ahmad na Ibn Maajah, Isnaad yake Hasan]