Du’aa Ya Swaalatul-Istikhaarah Ni Kabla Ya Salaam Au Baada Ya Kumaliza Swalaah?
Du’aa Ya Swaalatul-Istikhaarah Ni Kabla Ya Salaam Au Baada Ya Kumaliza Swalaah
SWALI:
Swalah ya Istikhara. Dua ya swalah ya Istikhara insomwa kabla ya kutoa salamu baada ya kutoa salam?
Shukran kwa kuyangalia maswali yangu na Jaza yako ikokwa Allaah
Jazaka Llah Kheir!
JIBU:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Du’aa ya Swalaatul-Istikhaarah inaweza kusomwa kabla ya kutoa salaam au baada ya kutoa salaam kwa kauli za ‘Ulamaa kama ifuatavyo:
Baada ya salaam ni rai ya Hanafiy, Maalikiy, Shaafi’iy na Hanbaliy.
Ama kusoma kabla ya salaam ni rai ya Shaykhul-Islaam Ibn Taymiyyah ambaye amesema kuwa inaruhusiwa kuisoma kabla au baada ya salaam. Inapendekezeka zaidi kuisoma kabla ya salaam kwani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akisoma du’aa nyingi kabla ya salaam na mwenye kuswali huwa bado yumo katika Swalaah kwa hiyo ni bora kuisoma du’aa humo.
Bonyeza kiungo kifuatacho upate faida ziyada:
Muda Wa Swalaah ya Istikhaarah
Na Allaah Anajua zaidi