Kauli Ya Swahaba Kuhusu Baadhi Ya Aayah Katika Qur-aan

 

 

Kauli Ya Swahaba Kuhusu Baadhi Ya Aayah Katika Qur-aan

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Sunayd bin Shakal amesema nimemsikia Ibn Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) akisema: Aayah Tukufu Kabisa katika Kitabu cha Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) ni:

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ۚ لَا تَأْخُذُهُ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ ۚ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ مَن ذَا الَّذِي يَشْفَعُ عِندَهُ إِلَّا بِإِذْنِهِ ۚ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ ۖ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَيْءٍ مِّنْ عِلْمِهِ إِلَّا بِمَا شَاءَ ۚ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ ۖ وَلَا يَئُودُهُ حِفْظُهُمَا ۚ وَهُوَ الْعَلِيُّ الْعَظِيمُ ﴿٢٥٥﴾

Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Aliyehai daima, Msimamia kila kitu. Haumchukui usingizi wala kulala. Ni Vyake pekee vilivyomo katika mbingu na vilivyomo katika ardhi. Nani huyu ambaye anashufai mbele Yake bila ya idhini Yake. Anajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawawezi kufikia kuelewa chochote kuhusu ujuzi Wake isipokuwa kwa Alitakalo. Imeenea Kursiyy Yake mbingu na ardhi. Wala hakumchoshi kuvihifadhi viwili hivyo. Naye ni Mwenye Uluwa; Ametukuka, Adhimu; Mkuu kabisa. [Al-Baqarah (2): 255]

 

 

Na Aayah iliyojumuisha khayr na shari ni:

 

 

إِنَّ اللَّـهَ يَأْمُرُ بِالْعَدْلِ وَالْإِحْسَانِ ﴿٩٠﴾

Hakika Allaah Anaamrishia uadilifu na ihsaan. [An-Nahl: 90]

 

 

Na Aayah yenye matumaini kabisa (ya maghfirah baada ya dhambi) ni:

 

 

قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾

Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu. [Az-Zumar (39:53)]

 

 

Na Aayah yenye uzito kabisa katika kumtegemea Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) ni

 

 

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا﴿٢﴾ وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ ۚ  

 

Na yeyote anayemcha Allaah; Atamjaalia njia ya kutoka (shidani). Na Atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.   [Atw-Twalaaq: 2 -3]

 

 

Masruwq akamwambia (Sunayd bin Shakal); Umesema kweli (kwamba kauli hiyo kasema Ibn Mas'uwd رضي الله عنه) [At-Twabaraniy 9:142]

 

 

 

 

 

Share