Baba Amefariki Ameacha Mjane, Ndugu, Watoto Na Anamiliki Nyumba

Baba Amefariki Ameacha Mjane, Ndugu, Watoto Na Anamiliki Nyumba

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Asalaam aleykum, mzee amefariki kaacha nyumba 1, ndugu wa kike 2, wa kiume 1, watoto wa kike 2 na mjane 1, nyumba itagawanywaje?

 

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

 

Awali ya yote ni kuwa lazima mwanzo ikiwa mzee ana madeni basi alipiwe na ikiwa aliacha wasiya basi pia utekelezwe lakini kiwango cha kutolewa kisizidi thuluthi (1/3).

 

Kwa hakika, inakuwa shida kuigawa nyumba kwa warithi hivyo wanaweza kuitia thamani hiyo nyumba kisha wakagawa kulingana na kiwango cha kila mmoja. Ikiwa si hivyo basi inatakiwa igawanywe vyumba na jambo hilo linakuwa ni vigumu ila tu iwe na vyumba vingi ambapo kila mmoja atapata sehemu yake. Kwa kuwa warithi ni wengi kiasi mara nyingi hutokea mtafaruku na hubidi nyumba ima kutiwa bei na kuuzwa au kununuliwa na mrithi mmoja kisha kila mmoja akapata sehemu yake.

 

Ama mjane kiwango chake kinafahamika vilivyo nacho ni thumuni kama Alivyobainisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَلَكُمْ نِصْفُ مَا تَرَكَ أَزْوَاجُكُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّهُنَّ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَهُنَّ وَلَدٌ فَلَكُمُ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْنَ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِينَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۚ وَلَهُنَّ الرُّبُعُ مِمَّا تَرَكْتُمْ إِن لَّمْ يَكُن لَّكُمْ وَلَدٌ ۚ فَإِن كَانَ لَكُمْ وَلَدٌ فَلَهُنَّ الثُّمُنُ مِمَّا تَرَكْتُم ۚ مِّن بَعْدِ وَصِيَّةٍ تُوصُونَ بِهَا أَوْ دَيْنٍ ۗ وَإِن كَانَ رَجُلٌ يُورَثُ كَلَالَةً أَوِ امْرَأَةٌ وَلَهُ أَخٌ أَوْ أُخْتٌ فَلِكُلِّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا السُّدُسُ ۚ فَإِن كَانُوا أَكْثَرَ مِن ذَٰلِكَ فَهُمْ شُرَكَاءُ فِي الثُّلُثِ ۚ مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصَىٰ بِهَا أَوْ دَيْنٍ غَيْرَ مُضَارٍّ ۚ وَصِيَّةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَلِيمٌ ﴿١٢﴾

Nanyi mtastahiki nusu katika walichoacha wake zenu ikiwa hawakuwa na mtoto. Na ikiwa wana mtoto, basi mtastahiki robo katika walichoacha, baada ya kutoa wasia waliyousia au kulipa deni. Nao wake zenu watastahiki robo katika mlichoacha ikiwa hamna mtoto. Na ikiwa mna mtoto basi watastahiki thumni katika mlichoacha, baada ya kutoa wasia mliousia au kulipa deni. Na ikiwa mwanamume au mwanamke anayerithiwa hana mtoto wala wazazi, lakini anaye kaka au dada, basi kila mmoja kati yao atastahiki sudusi. Na wakiwa ni wengi ya hivyo basi watashirikiana katika theluthi, baada ya kutoa wasia uliousiwa na kulipwa deni pasipo kuleta dhara.  Huu ni wasia kutoka kwa Allaah, na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mvumilivu. [An-Nisa: 12]

 

 

Ndugu wa kiume na wa kike wa aliyefariki watarithi pia kwa kuwa aliyefariki hakuacha mtoto wa kiume. Kwa hiyo, binti 2 wa aliyefariki watapata kila mmoja thuluthi.

 

Jadwali ya wirathi itakuwa kama ifuatavyo:

 

 

Namba

 

Uhusiano na Aliyefariki

 

Kiwango

 

Asilimia

1

Mjane

Thumuni (1/8)

12.5

 

2

Binti 1

Thuluthi (1/3)

33.33

 

3

Binti 2

Thuluthi (1/3)

33.33

 

4

Kaka

 

10.42

 

5

Dada 1

 

5.21

 

6

Dada 2

 

5.21

 

 

Jumla

 

100.00

 

 

 

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

Share