Katelesi Za Nyama Za Kotmiri
Katelesi Za Nyama Za Kotmiri
Vipimo:
Viazi - 3 LB
Nyama - 1 LB
Unga wa mkate (Breadcrumbs) - 1 kikombe cha chai
Mayai - 2-3
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Vipimo Vya Nyama:
Tangawazi na kitunguu saumu(thomu) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Chumvi - Kiasi
Jeera (Bizari ya pilau ya unga) - 1 kijiko cha chai
Dania (Gilgilani ya unga) - 1 kijiko cha chai
Pilipili manga ya unga - 1 kijiko cha chai
Mdalasini wa unga - ¼ kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Ndimu au limau - 2 vijiko vya supu
Kotmiri iliyokatwakatwa (chopped) - Msongo 1 kamili au zaidi yake.
Kitunguu kilichokatwa katwa (chopped) - 1 Kikubwa
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha Viazi, vikiwiva menya maganda na viponde.
- Weka nyama katika sufuria ndogo, ichanganye na vitu vyake vyote isipokuwa kotmiri na vitunguu.
- Ipike nyama mpaka ikauke.
- Tia Kotmiri na vitunguu viliyokatwakatwa, changanya weka kando.
- Chukua viazi viliyopondwa Changanya na hiyo nyama.
- Fanya madonge kiasi katika mkono ufanye viduara.
- Tayarisha katlesi zote hivyo hadi umalize viazi na nyama.
- Weka mafuta katika karai yapate moto sawa sawa.
- Chomva katlesi katika mayai uliyoyapiga sawa sawa kisha garagaza katika unga wa mkate (breadcrumbs) na uzikaange mpaka zigeuke rangi.
- Epua weka katika karatasi ya inayokunwa mafuta (Kitchen paper) au weka katika chujio zichuje mafuta.
- Tayari kuliwa.