Juisi Ya Nanasi Na Tango
Juisi Ya Nanasi Na Tango
Vipimo
Nanasi - 6 slesi
Tango - 1 la kiasi
Sukari - ½ Kikombe
Barafu - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha
- Katakata nanasi na tango vipande vipande.
- Kisha tia kwenye mashine ya kusagia pamoja na sukari na vipande vya barafu.
- Ikiwa nzito sana ongeza maji.
- Mimina katika gilasi
Kidokezo
Vipimo hivi ni kupata takriban gilasi 6.