Sharbati Ya Maziwa Na Lozi
Sharbati Ya Maziwa Na Lozi
Vipimo
Juisi ya barafu (frozen juice)
yoyote upendayo - 1 Pakitti
Maziwa - 3 gilasi
Sukari - Kiasi
Lozi - ¼ Kikombe
Strobberri - Kiasi ya kupambia
Namna Ya Kutayarisha
- Katika mashine ya kusagia (blender) tia Juisi ya barafu, maziwa, lozi na sukari kisha saga hadi ichanganyike vizuri.
- Ikiwa nzito sana unaweza kuongeza barafu ukipenda.
- Mimina katika gilasi, pambia strobberri na itakuwa tayari.
