Hikma Ya Yanayopasa Na Yasiyopasa Katika Hedhi Kuhusu Swalaah na Swawm

 

Hikma Ya Yanayopasa Na Yasiyopasa Katika Hedhi Kuhusu Swalaah na Swawm

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI

 

Assalam aleikum warahmatullah wabarakatu,

Inshaallah ulifunga mwezi wa ramadhan kwa kheri na barka.  Ya rabi atutakabaliye saumu zetu na dua zetu na atughufuriye dhambi zetu, Amin.

I just have couple questions and will appreciate if you can help me  out inshaallah.
 
Why is that when a woman is on her periods, she is not allowed to fast, read or even touch qur'an?  I understand  it's because one is not considered to be "clean" during  that time.  However, si ni Allaah Mwenyewe ndiye alieumba  wanawake kupata periods?  Why can we not
pray to him then when we are on our periods?   Why then do we also have to pay back for the days that we  didn't fast?
 
Saa nyengine hujaribu kuwaelezea non muslims how certains things are perceived in Islam but mara nyengine hushindwa  kwa vile mimi
mwenyewe huwa sina jawabu.

Nitashukuru sana kama utaweza kunielezea zaidi juu ya habari hii.
 
Fil amanillah

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Muumini inampasa aamini na kuwa na yakini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni Mwenye hikmah na kwamba  Anapoamuru jambo lolote, basi Huamuru kutokana na hikmah yenye upeo wa hali ya juu kabisa, na Haamrishi jambo ila litakuwa kwa sababu lina  manufaa kwa mwana Aadam na Hakatazi jambo isipokuwa tu litakuwa kwa sababu  lenye kuwahifadhi wana Aadam kutokana na mauovu na madhara.

 

Kuhusu hedhi na kusoma Qur-aan:

‘Ulamaa wamekhitilifiana kuhusu jambo hili; wako wanaosema haijuzu na wako wanaosema inajuzu. Kauli inayokubalika zaidi hakuna makatazo ya kumzuia mwanamke asisome Qur-aan akiwa katika hedhi. Kwa maelezo bayana, tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho:

 

Kushika Na Kusoma Qur-aan Katika Hedhi, Nifaas Na Janaba

 

Kuhusu makatazo ya Swawm.

 

Ni rahmah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kwa wanawake, kwani wanapopoteza damu nyingi katika hedhi huwafanya wawe dhaifu. Kwa hiyo atakapofunga mwanamke akiwa katika hedhi atazidi kuwa dhaifu kutokana na hedhi na kufunga na hii itakuwa ni jukumu lenye kuzidi uwezo wake na huenda likamletea madhara.   [Shaykhul-Islaam ibn Taymiyyah Maj'muw Al-Fataawa 25/234]

 

Ama kulipa deni la Swawm na kutokulipa Swalaah ni amri kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kama  ilivyothibiti katika Hadiyth:

  

عن عَائِشَة رضي الله عنها: كُنَّا نَحِيضُ عَلَى عَهْدِ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَنُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّوْمِ  وَلا نُؤْمَرُ بِقَضَاءِ الصَّلاةِ   مُتَّفَقٌ عَلَيْه

Imepokelewa kutoka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaahu ‘anhaa) kwamba, tulikuwa katika hedhi wakati wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)   tuliamrishwa kulipa swawm lakini hatukuamrishwa kulipa Swalaah))  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 عن أَبُو سَعِيدٍ : قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم : (( َلَيْسَ إحْدَاكُنَّ إذَا حَاضَتْ لَمْ تُصَلِّ وَلَمْ تَصُمْ  فَذَلِكَ مِنْ نُقْصَانِ دِينِهَا)) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ

 

Imepokelewa kutoka kwa Sa’idy kwamba: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je, Haijakuwa kwamba mmoja wenu anapokuwa katika hedhi haswali wala hafungi?  Hii ndio maana ya kuwa mmepungukiwa (wanawake) na Dini (yaani kupungukiwia baadhi ya hukmu)  [Al-Bukhaariy]

 

  

 

Ama kuhusu mwanamke kumdhukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) akiwa katika hedhi kama kuomba maghfirah na du’aa, kumsabbih Allaah, Kumkabbir na kadhaalika inajuzu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

 

 

Share