Swiyghah (Maneno) Ya Wakati Wa Kufungisha Ndoa Ni Yepi?

SWALI:

 

Asalaam alaykum,

nimepewa jukumu kutoka kwa baba na mama wa mtoto wa kike kumuozesha mtoto wao kwa ndugu yangu wa kiume lakini sijui (sigha,matamshi) ya kuozesha watu wawili wametakana kwa sunna ya M. Mungu na mtume wake (s.w.a).

(1) Baba na mama wa mtoto wa kike wameniomba kitu hiki na watahudhuria ndoa.

(2) Mtoto wa kike miaka 24 na amemkubali mwanamme kwa radhi zake.

(3) Mtoto wa kiume ni miaka 27 na amemkubali mtoto wa kike kwa radhi zake.

(4) Mashahidi waliopo ni kaka zangu, na haloo zangu.

washukran.

 


JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea na kivivu

 

Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Swiyghah (au maneno) yanayosemwa katika ndoa. Ikiwa hayo masharti yote yamekamilika basi utasoma khutba ya nikaha kama ifuatavyo:

 

1.     Innal Hamda Lillaahi Nahmaduhu wa Nasta‘iynuhu wa Nastaghfiruhu wa Natuwbu ilayhi. Wa Na‘udhu Billaahi min shuruuri anfusina wa sayyi’ati a‘maalina man yahdihi Allaahu falaa mudhwilla lahu wa man yudhwlil falaa haadiya lahu wa Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaahu wa ash-hadu anna Muhammadan ‘abduhu wa Rasuuluhu.

 

2.     Baada ya hapo utasoma Surah 3, Aayah ya 102;

 

3.     Surah ya 4 Aayah ya 1 na

 

4.     Surah 33, Aayah ya 70 – 71.

 

5.     Kisha utawahimiza waliohudhuria na haswa vijana kuoa kwani hiyo ni Sunnah ya Manabii na watu wema. Pia uwaonye Waislamu wasiwe ni wenye kuiendea zinaa kwani hiyo ni njia mbaya zaidi (17: 32).

 

6.     Baada ya kumaliza mawaidha hayo mafupi utamshika mkono bwana harusi na kumwambia: Zawwajtuka fulaan binti fulaan bimahriha kamat tafaktum au bimahriha kadhaa (kwa Kiswahili unaweza kumwambia Nimekuoza wewe fulani binti fulani [utaje jina la binti pamoja na la babake] kwa mahari mliyosikilizana au kwa mahari kadhaa [utaje kiwango cha mahari]). Bwana harusi naye atajibu kwa kusema: Nimekubali kumuoa fulani binti fulani kwa mahari yake…

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share