Baba Na Mtoto Wamepeleka Posa Kwa Msichana Mmoja Bila Ya Kujua – Yupi Mwenye Haki Zaidi Kumuoa?
SWALI:
Kuna mschana amechanganyikiwa. katika masomo yake alikutana na mvulana wa kiisalmu na yule mvulana kumuona huyo binti akampenda, akamuambia binti kuwa mm nitakuja kukuposa, binti hakujibu kitu, baada siku mbili binti akakutana na mzee, mzee huyo pia akampenda akamuambia nataka kuja kukuowa, binti hakujibu kitu, basi huyo kijana akaenda kwanza kupeleka posa akaambiwa atajibiwa, kisha yule mzee pia akapeleka posa pia akaambiwa atajibiwa, kukichunguzwa kumbe yule mzee na mtoto ni baba na mwana. Sasa huyu binti ataka ushauri amkubali yupi? Amechanganyikiwa.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuposwa msichana na baba na kijana wake.
Hakika katika sheria yetu inatakiwa inapoletwa posa basi mtu akiwa anajua ikiwa posa imepelekwa asipeleke posa juu ya posa nyingine. Na lau atakuwa hajui
Kwa kuwa kijana alikuwa tayari ameleta posa ilikuwa wazazi wa msichana wasikubali posa nyingine mpaka wajibu ile ya kwanza kwani tayari walikuwa wametoa kauli kuhusu
Vilevile huyo binti kusema kuwa alikuwa ameshapewa taarifa na kijana huyo kuwa atakwenda kupeleka posa. Ilikuwa ni wajibu wake atoe maoni yake kwa wazazi na maamuzi yachukuliwe. Na alipokwenda baba naye akanyamaza, basi inaonyesha huyo binti hajui analotaka au anaweza kuwa kapata kishawishi fulani ambacho kimemfanya asiwe na maamuzi ya kukata.
Ni bora wazazi watoe maamuzi haraka
Na Allaah Anajua zaidi