Kijana Kaweka Ahadi Na Msichana Kuoana, Posa Imekuja Msichana Kakataa, Inafaa Hivyo?
SWALI LA
Assalamu alamualaykum,
Mimi ni kijana wa kiume ambae sijawahi kuoa, lakini inshaallah ninayo matarajio hayo. Imetokezea kuzungumza na msichana fulani kuhusu mas-ala ya kuoana baada ya muda fulani, ambapo mimi nitakuwa nishajitayarisha na jambo hilo, lakini wakati tunasubiri mimi na huyo msichana huo muda ufike pametokea posa nyengine kabla ya mimi na hapo msichana huyo alikataa katakata kuolewa na mtu huyo na alipoulizwa jee unae mtu ambae mmekubaliana akasema ndio na akanieleza mimi na mimi nikakubali kufanya mawasiliano na wazee wake na wakakubali jambo hilo, lakini huo muda wetu haujafika. Jee mimi nilifanya kosa katika hali
Na pia wazee hao katika hali
SWALI LA PILI:
Mwanamke kaposwa lakini kakataa kwa sababu anamchumba wake wameahidiana kuoana, na alipoulizwa amlete huyo kijana alikwenda na kazungumza na wazee wa msichana na wakakubali lakini alitaka apewe muda wa miaka 2 ili ajitayarishe. Swali ni: Jee kijana huyu alikosea kufanya hivyo na hali ya kuwa hawakufanya matendo machafu? Na jee katika uislamu inafaa kueke ahadi
JIBU
:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kijana kumposa msichana na kuomba muda ili ajitayarishe.
Posa kama hiyo haina tatizo kabisa kukiwa na udhibiti kwa hao walioposana kulingana na Shari’ah. Udhibiti huo ni kutowasiliana wala kukutana mukiwa peke yenu, wala kutembea pamoja, wachumba wawe wakweli kati
Msichana ana haki ya kumkataa mvulana mwengine kwa sababu moja au nyingine –
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimposa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) na kumuoa baada ya miaka mitatu. Kwa hiyo, posa na kupatiana muda hakuna tatizo kabisa katika Shari’ah. Hivyo, ahadi kama hizo hazina tatizo katika Dini lakini muweze kutekeleza
Na Allaah Anajua zaidi