Yuko Mbali Na Anayetaka Kumchumbia Je, Inafaa Kuongea Naye Kabla Ya Ndoa?

SWALI:

 

Assalamualeikum

Bismillahirrahmanirrahim

 

 

Alhamdulillah, mimi ni mwanamke wa miaka 21, nna kazi yangu na nipo masomoni kusomea hiyo kazi. Nina mchumba wangu hayupo hapa, yupo ulaya anatafuta maisha na ameshakuja kuleta wazee wake kwa wazee wangu lakini bado haijakubalika sababu wamesema wanataka miaka minne kwa ajili ya matayarisho ya kazi na kimaisha ya huyu mwanamme...jee inafaa mimi kua naongea nae? Na pia kupeana ushauri wa maisha yanavokwenda? Je inafaa? Wabillahi tawfiq

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kuongea na mchumba wako ambaye amekataliwa na wazee wako. Mazungumzo baina ya mwanamme na mwanamke ni njia moja ya kukaribia zinaa, hiyo ni kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katujulisha kila kiungo cha mwanaadamu kinazini, mdomo ukiwa ndani ya tangazo hilo. Na Allaah Aliyetukuka Ametunasihi kuwa tusikaribie zinaa (al-Israa’ [17]: 32).

 

Na kulingana na swali lako wazee wako wamekataa posa mpaka baada ya miaka minne wakati ambao mchumba wako atakuwa amestakiri kimaisha. Kwa hiyo, wewe na yeye hamna hata hayo mahusiano ya uchumba. Kwa ajili hiyo, ni bora msiwe mkizungumza kungojea wakati atakapokuja tena na kuposa na kukubaliwa. Hata ikiwa amekubaliwa ni bora kuchukua tahadhari kubwa katika mazungumzo.

 

 

Kukubaliwa posa kwa mwanamme si kibali cha kuzungumza mnayotaka kwani hajakuwa mumeo. Kile kinachokubaliwa baada ya posa ikibidi ni yale mawasiliano ya muhimu yenye kuhusiana na masuala ya muhimu ambayo yasiyoingiliana na mapenzi na hisia ili Shaytwaan asiingie kati yenu.

 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi

 

Mawasiliano Na Mchumba Baada Kuposa Na Kabla Ya Ndoa

 

Anaweza Kuzungumza Na Kuonana Na Aliyemposa?

 

Asubiri Kumaliza Shule Kuolewa Au Aendelee Kuwa Na Mahusiano

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share