Kuna Uhalali Wa Mzazi Kumlipa Mtoto?
SW
Ni aya gani katika Quran inayoelezea uhalali wa mzazi kumlipa mtoto wake.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uhalali wa mzazi wa kumlipa mtoto. Hatujapata kuona katika Qur-aan Aayah yoyote inayoeleza kuhusu uhalali wa mzazi kumlipa mtoto wake. Imekuja katika Hadiyth Sahihi kuwa mtoto mmoja alikwenda kumshitaki babake kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa amechukua vitu vyake. Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimwambia kuwa vitu vyako na wewe mwenyewe ni wa babako.
Kisha ni utovu wa nidhamu na adabu kwa mtoto kumshika babake amlipe kwa alichompatia. Inapasa kutambua kwamba vyovyote itakavyokuwa, mtoto hawezi kuwalipa wazazi wake, tabu zao zote za kumzaa, kumlea na kumuongoza. Hali kadhalika baba naye haifai wala haipendezi kumdai mwanae, ila
Na Allaah Anajua zaidi