Dehii Baree - Bajia Katika Mtindi (Pakistani)
Dehii Baree - Bajia Katika Mtindi (Pakistani)
Vipimo
Maash daal (hadesi/chooko nyeupe za kupaazwa) - 3 vikombe
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 5 chembe
Pilipili mbichi - 1
Chumvi - kiasi
Jiyrah (bizari ya pilau) - 1 kijiko cha chai
Baking Powder - 1 kijiko cha chai
Mtindi (Yoghurt) - 750 gms
Sukari - 2 vijiko vya supu
Kitunguu majani (spring onion) - 3 miche
au kitunguu cha kawaida kimoja)
Viazi - 3
Dengu (chick peas) - 1 kikombe
Mafuta ya kukaangia - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka maash daal usiku, siku ya pili, tia katika mashine ya kusagia (blender) saga pamoja na kitunguu thomu, chumvi, pilipili mbichi, jiyrah, kwa maji kiasi tu ya kusagia kama unavyosaga bajia za kunde.
- Mimina katika bakuli tia baking powder changanya vizuri.
- Teka kwa mkono au kijiko kiasi na choma kama bajia, kisha zichuje mafuta na weka kando.
- Tia maji yalilyo dafu dafu (warm water) katika bakuli na umimine bajia.
- Kamua bajia zitoke maji na ziweke kando tena.
- Chemsha viazi ukatekate vipande vidogo vidogo.
- Chemsha dengu baada ya kuroweka au tumia za tayari katika kopo.
- Katika bakuli la kupakulia, tia mtindi, sukari, chumvi kidogo sana, na maji kiasi ya glass moja uchanganye vizuri sana uwe mwepesi kiasi.
- Katia katia kitunguu, tia viazi na dengu.
- Mimina bajia katika mtindi zichanganyike na sosi ya mtindi bila ya kuzivuruga.
- Kaanga jiyrah nzima (Bizari ya pilau) kidogo katika kikaango kisha isage kidogo na nyunyizia juu ya dehii baree (kama ilivyo katika picha) pamoja na pilipili ya unga nyekundu ukipenda, zikiwa tayari kuliwa na chatine ya mtindi na nana na ukwaju.
Mapishi Ya: