Kula Samaki Ijumaa Na Kukaribia Zinaa
Kula Samaki Ijumaa Na Kukaribia Zinaa
Swali:
Assalam Ayekum viongozi wa dini yenye haki ya Allaah s.a, swali langu ni kwamba kuna ayaah /hadiyth ya mashia nimeisikia kwamba '" mtu anayekula samaki siku ya ijumaa nanaingia peponi na nyingine usiikaribie zinaa ila kwa dharura.
Jibu:
AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.
Hadiyth za Mashia ni za kwao lakini cha kufahamika ni kuwa sisi na wao tunatafautiana kabisa katika Itikadi, na vitabu wanavyotumia wao vya Hadiyth sisi hatuvitambui na wao hawawatambui kabisa Maimamu kama Al-Bukhariy, Muslim na wengineo.
Hivyo, wao wanaweza kusema chochote wanachotaka, kwao hata huyo samaki ni lazima achinjwe kabla ya kuliwa (kama wanavyosema Ma-Bohora, ambao ni tawi la kishia).
Kwa hakika katika Uislamu wa sawa hata ukiwa katika Ihramu ambapo hufai kuwinda mnyama lakini inaruhusiwa kuvua samaki. Na katika Hadiyth Sahihi hakuna kuwa ukila kitu fulani siku fulani basi wewe umepata cheti cha kuingia Peponi au ndio utaingizwa motoni. Isipokuwa tu kwa kula vitu ambavyo ni haramu ndio utapata dhambi.
Na kuhusu zinaa, zinaa ni zinaa wala hakuna zinaa ya dharura. Allah Ametueleza kuhusu jambo hili kiujumla pale Aliposema:
وَلَا تَقْرَبُوا الزِّنَىٰ ۖ إِنَّهُ كَانَ فَاحِشَةً وَسَاءَ سَبِيلًا ﴿٣٢﴾
Na wala msiikaribie zinaa. Hakika huo ni uchafu na njia mbaya kabisa. [Al-Israa: 32].
Hapa Allaah Ametukataza hata kuikaribia. Hawa Mashia huwa wanajuzisha zinaa kwa jina ndoa ya muda (Mut'ah) ambayo imeharamishwa. Na ukiangalia katika tovuti yetu hii kwenye kiungo kiufatacho, ingia utapata maelezo marefu kuhusu aina hiyo ya zinaa ambayo imepigwa marufuku na Uislamu.
Na Allah Anajua zaidi.